Imeelezwa kuwa, matumaini ya kufikiwa makubaliano baina
ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23
yamefutika kufuatia hatua ya Umoja wa Mataifa ya kubadilisha jukumu la
askari wa kofia bluu wa umoja huo huko Kongo. Gazeti la Potentiel la
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linaripoti kwamba, hatua hiyo ya Umoja
wa Mataifa imepunguza uwezekano wa serikali ya nchi hiyo kutiliana saini
makubaliano ya amani na waasi wa Machi 23. Kwa mujibu wa azimio nambari
2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa askari wa kofia bluu wa
Umoja wa Mataifa sasa wana ruhusa ya kufanya operesheni za kijeshi dhidi
ya waasi wa M23 na kwa msingi huo wameondoka katika nafasi yao ya kuwa askari wa
kulinda amani na kuwa vikosi vya kupambana na waasi. Hatua hiyo ya Umoja
wa Mataifa imetajwa kuwa imefuta kabisa uwezekano wa kufikiwa
makubaliano ya amani baina ya waasi wa M23 na serikali ya Kinshasa.
Aidha wiki iliyopita Uganda ilishindwa kuikurubisha pamoja mitazamo ya
waasi wa M23 na wawakilishi wa serikali ya Kinshasa katika mazungumzo ya
Kampaka.
No comments:
Post a Comment