May 5, 2011

LULU, SALAMA JABIR WABAMBWA

MASTAA wawili wanaotamba katika nyanja tofauti, Salama Jabir na Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani) wamebambwa ndani ya New Maisha Club, Msasani jijini Dar es Salaam wakifanya mambo ya ajabu, Gazeti la Risasi Jumatano linakudondoshea moja moja.

Mastaa hao wenye majina makubwa, walikuwa wamekaa katika meza moja kama wapenzi huku wakifanya vitendo vilivyovuka mipaka na kuwafanya wadau wa burudani kutafsiri kwamba vilikuwa ni vya kisagaji.

Mapaparazi wetu waliokuwemo ukumbini humo siku hiyo ya Jumapili ya Pasaka, walipigwa na butwaa na ukaribu wa wawili hao ambapo walishtushwa zaidi na maneno ya watu waliokuwa wakimuonea huruma Lulu.
“Kwanza bado mdogo na anapokaa na watu kama akina Salama tulitegemea angefunzwa maisha lakini ndiyo kwanza anafundishwa vitu vya ajabu,” alisema mmoja wa watu waliokuwepo ukumbini humo.

Labda kwa kuwa Lulu na Salama walikuwa hawasikii kile kilichokuwa kikisemwa, waliendelea kuzungusha raundi za vinywaji kwa fujo bila kujali kuwa mmoja wao ni ‘sidanganyiki’ hali iliyozidi kuzua viulizo vingi kwa watu waliokuwa wakiwatazama.

Aidha, baada ya pombe kuwakolea walizidisha vituko na kuonesha kwamba wao ni damu damu na wala hawakuwa na haja ya kumuonea noma na mtu yeyote.

Salama aliyekuwa akipuliza sigara ndiye aliyekuwa kinara wa zoezi hilo kwa kumfanyia vimbwanga hivyo Lulu huku akimshika sehemu mbalimbali ambazo ni hatarishi kwa mwanamke.

Hali hiyo ilisababisha taa nyekundu kuwaka vichwani mwa waandishi wetu, hivyo kuongeza umakini kufuatilia kila walichokifanya ili kujua hatma ya sinema hiyo ya bure.

Salama aliyewahi kutamba na kipindi cha Planet Bongo cha Runinga ya EATV alimfanya Lulu alegee mithili ya mtu aliyetafuna kungu ndipo mapaparazi wetu walishindwa kuvumilia wakaamua kuwafuata na kuwahoji.

Mmoja wa mapaparazi wetu aliwauliza kulikoni hadi walifikia hatua hiyo ndipo Salama aligeuka mbogo na kuanza kushusha mvua ya matusi na kejeli kama siyo dharau.

“Aaah, jamani sisi tuko bize na mambo yetu, vipi tena tunaanza kufuatiliana hadi sehemu za starehe siyo ustaarabu kabisa, kila mtu afuate mambo yake,” hayo yalikuwa ni baadhi ya maneno ya kistaarabu yaliyotoka kinywani mwa Salama.

Paparazi mwingine alipomuuliza Lulu alikuwa akifanya nini na Salama, akamjibu kama alivyosema Salama.

No comments: