Dec 27, 2013

HIVI NDIVYO LIVYOKUWA SIKU YA CHRISTMAS PANDE ZA KAHAMA TENGUA KAULI NA BROTHER K WA FUTUHI
Hii ilikuwa ni jana mchana katika viwanja vya Masabo mjini Kahama ambapo walikuwepo Brother K na sharobaro wa Kihaya kutoka FUTUHI ya Star TV Pamoja na Chili na Ringo kutoka Vituko show ya Chanel Ten.

Show hii imeandaliwa na redio kahama FM, na kuwashirikisha watoto pamoja na watu wazima yani show ya kifamilia zaidi.

Umati wa watu walioshuhudia show hiyo
Moja kati ya Mchezo waliouonesha wote kwa pamoja
Wadau wa Kahama fm wakiangalia show
Kulikuwa na nyomi si mchezo
Brother K, Chili na Sharo la kihaya
Chili aliyekaa na Ringo anayevizia kwa pembeni wakifanya yao

Pombe noumaa!!! KONYAGI YAUA MFANYAKAZI WA TIGO SIKU YA KRISMASI...!!


Mwanamme aitwayeGodi Shaini Fanuel Mangala (34)  mkazi wa mtaa wa Majengo Mapya  kata ya Ngokolo mjini Shinyanga amefariki dunia kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni kunywa
pombe aina ya konyagi kupita kiasi.

Mashuhuda wa tukio hilo wameimbia malunde blog kuwa tukio hilo la kusikitisha limetokea siku ya krismasi  Desemba 25 mwaka huu saa moja jioni.

Wamesema marehemu alikuwa anakunywa pombe na wenzake katika  moja ya Glosary mjini Shinyanga na  baadaye mwenzao alizidiwa na kulazimika kurudishwa nyumbani kwake ili akapumzike na hali ilipozidi  kuwa mbaya wakampeleka katika hospitali ya mkoa lakini akafariki dunia akiwa njiani

Hata hivyo mmoja wa  mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa anashindana na wenzake kunywa pombe maarufu konyagi ama wengine wanapenda kuziita Bapa.

Diwani wa kata ya Ngokolo mjini Shinyanga kulikotokea tukio hilo Sebastian Peter amesema kifo cha God ni mipango ya mungu kutokana na kwamba marehemu hakuwa mgeni wa pombe na kwamba inadaiwa kuwa kabla ya kifo hicho marehemu alikuwa analalamika kusumbuliwa na vichomi siku hiyo.

Akizumgumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa alikiri kuupokea mwili  wa marehemu muda wa saa moja jioni Desemba 25 mwaka huu,akiwa tayari amefariki dunia na kesho yake Desemba 26 ndugu wa marehemu walifika hospitalini hapo na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi hivyo kushindwa kufanya uchunguzi wa kitaalamu ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema bado hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki wa karibu na marehemu anayejulikana kwa jina la John tayari mwili wa marehemu God Shaini umesafirishwa kwa ajili ya mazishi hapo kesho nyumbani kwa mama yake  Mabatini mkoani Mwanza.

"Mkorogo Umenitia Adabu sana"...Wema Sepetu..!!


MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia  mwilini mwake.
Wema Sepetu
Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema  kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.

NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.

ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.

Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.

AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.

Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya  wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.

ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.

Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.

Jul 10, 2013

ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI WAGOME KUILIPA KODI YA SIMU YA SH. 1000.....AMEDAI KUWA KODI HIYO ILIPITISHWA KINYEMELASakata  la  kodi  ya  line  ya  simu  limeendelea  kuwakuna wanasiasa  wetu  ambao  wamekuwa  wakifunguka  kwa  nyakati  mbalimbali  kupitia mitandao  ya  kijamii....

Baada  ya  January  Makamba, Zitto  kabwe  naye  amefunguka  na  kudai  kuwa  kodi  hiyo  ni  batili  na  ilipitishwa  kinyemela  kwa  sababu  ilikuwa  imeshaondolewa....

Huu  ni  ujumbe  wake  aliouweka  katika  account  yake  ya  facebook:
Baada ya  kauli  hiyo,Zitto  Kabwe  aliandamwa  na  maswali  mengi  sana  toka  kwa  wananchi  wakidai  kuwa  "Makamba  alisema  tuwalaumu  ninyi  maana  ninyi  wabunge  ndo  mlibariki  kodi  hii"

Zitto  naye  alishindwa  kulijibu  swali  hilo  na  kuwataka  wananchi  "wachukue  simu  zao, wawapigie  wabunge  wao  wawaulize  ni  kwa  nini  walipitisha  kodi  hii"

 "Anasema  hiyo  kwa  sababu  wabunge  ndio waliopitisha.Wabunge  ndio  wawakilishi  wa  wananchi.Jambo likipita bungeni hao ndio wa kwanza kulaumiwa.Yupo sahihi kabisa.Mpigie mbunge wako simu muulize kwa nini  alikubali au  hakupinga kodi hii"..Hili  ni  jibu  za  Zitto Kabwe

JANUARY MAKAMBA AWATAKA WANANCHI WAWALAU WABUNGE WAO KUHUSU KODI YA 1000 KWA KILA LAINI.....ADAI WIZARA YAKE ILIPINGA VIKALIHaya  ni  majibu ya  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba akijibu maswali katika mtandao wa Twitter kuhusu kodi mpya ya TZS 1000 kwa mwezi kwa kila line ya simu. 


  •  Amesema kwamba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliipinga kodi hiyo.

  •  Amesema kwamba Hazina (Wizara ya Fedha) walikubaliana na maoni ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuhusu kodi hiyo.
  • Amesema kwamba Bunge ndilo lililopitisha kodi hiyo na si Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

"NITAENDELEA KUPAMBANA NA WABISHI WASIOTAKA KUHAMA ILI KUPISHA MIRADI YA UJENZI"...MAGUFULIWAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli ameapa kupambana kwa kuwabomolea au kuwakomesha kwa njia nyingine, watu waliogoma kuhama kwa ajili ya kupisha miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na wizara yake.

Katika hilo, tayari amekwishatangaza uamuzi mzito wa kuruhusu kampuni ya ujenzi ya Jaspal Singh, kujenga barabara kwa kiwango cha lami kwa kuzizunguka nyumba za wakazi waliogoma kuhama na kukimbilia mahakamani akiamini kuwa wataondolewa kwa kugongwa na malori yatakayokuwa yakipita baada ya barabara hiyo kukamilika.

Pamoja na hilo, Dk. Magufuli amesema atazibomoa bila kulipa fidia nyumba za wananchi nane waliokataa kufanyiwa tathmini ili kupisha mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, endapo hawatabadili msimamo wao huo.

Uamuzi huo aliutangaza jana baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo alibaini kuwa miradi mingi inakwamishwa na wananchi wa maeneo husika.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Kigogo hadi Jangwani yenye kilomita 2.7, alishangazwa kuona mradi umesimama huku vifaa vikionekana kuwa na kutu kitendo ambacho kilimlazimisha ahoji.

Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Mussa Ali pamoja na Mkandarasi Jaspal Hungh, walimueleza Magufuli kwamba kuna wananchi wenye nyumba 16 wamechukua fidia na kufungua kesi mahakamani kwa kudai kiasi walichopewa ni kidogo.

Aliongeza kuwa kesi hiyo imechukua zaidi ya miaka miwili bila kutolewa hukumu na kusababisha mradi kukwama.

TAMKO LA KIGOGO

Akizungumzia hilo Magufuli alisema: “Naomba tusiingilie mahakama lakini naagiza kuanzia leo (jana), anzeni kujenga barabara ya lami kwa kuzizungushia lami nyumba hizo na kuruhusu gari zipite, nadhani haitapita wiki kabla hazijagongwa na malori ya mchanga, sitaki kusikia Serikali inadaiwa fidia ya ucheleweshaji wa mradi.

“Pia naagiza kwamba mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kwamba meneja wa mradi fungua kesi dhidi ya wananchi hao waliochukua fedha za fidia na kwenda mahakamani, huo ni wizi.

“Serikali ikishinda kesi ya madai yao ya fidia ndogo, wao ndio watawajibika kujenga sehemu ya nyumba zao, hatuwezi kuchezea fedha kwani kuwafidia Sh bilioni 3.8 ambapo mradi wenyewe unagharimu Sh bilioni 7.6.

“Kuna mazoea yameibuka ya watu kuchezea Serikali na mahakama, sasa nasema katika miradi ya wizara yangu nitapambana nao watu wenye kiburi cha kuchezea vyombo hivyo,” alisema.

DARAJA L A KIGAMBONI

Awali akitembelea eneo la Kigamboni uliko mradi wa daraja la Kigamboni, Magufuli aliwataka wananchi nane waliokataa kufanyiwa tathmini ya nyumba zao ili kupisha mradi huo, kubadili msimamo wao haraka kabla ya Serikali haijazibomoa nyumba hizo kwa nguvu tena bila kulipwa.

Jumla ya watu 121 walitakiwa kuhama kupisha mradi huo ambapo kati yao 113 walikubali kufanyiwa tathmini na kulipwa jumla ya Sh bilioni 11.7, lakini nane walikataa.

“Nasema Serikali ikiamua kufanya ukorofi utakuwa mkubwa kuliko msimamo wako, sasa nasema hao waliokataa kufidiwa naomba wasiambulie patupu kabla hatua hazijachukuliwa, wakubali kuchukua kiasi kitakachothaminiwa haraka, sisi tukija tutabomoa na hatukulipi na mradi utaendelea.

“Naomba daraja hili likamilike na kukabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete Januari 31, 2015 na kulifungua, sitaki kuona linafunguliwa na rais mwingine ambaye anaweza kusema yeye ndiye aliyejenga wakati ni uongo, aliyeweka jiwe la msingi ndiye atakayefungua,” alisema.

Mradi wa daraja la Kigamboni unagharimu Sh bilioni 214 na kati hizo asilimia 40 zinatolewa na Serikali wakati Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unachangia asilimia 60.

Mbali na hilo, Dk. Magufuli ameagiza kuondolewa haraka wakazi wa eneo la Davis Corner, Temeke ambao licha ya kulipwa fidia ili kupisha ujenzi wa barabara ya Jet Corner hadi Temeke, wameshindwa kuhama mpaka sasa na badala yake kutumia fedha hizo kuendeleza ujenzi na kudai malipo mengine.

Magufuli alishangazwa kuona wananchi hao ambao wamegoma hadi sasa wamelipwa fidia Sh 15.8 huku mradi wenyewe ukiwa Sh bilioni 12 na barabara ikiwa haijakamilika.

Mradi wa mabasi ya kasi

Akikagua mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam (DARTS), Magufuli alifurahishwa na kasi pamoja na kiwango cha ujenzi wa mradi huo, ambao utapunguza msongamano wa magari.

Meneja wa mradi wa Darts, Baraka Ally alimweleza Dk. Magufuli kwamba mradi unaendelea vizuri na utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Hata hivyo alisema changamoto kubwa inayoukabili mradi huo ni uvamizi wa wafanyabishara ambao wamekuwa wakiweka biashara zao barabarani huku wenye teksi na magari mengine wakiegesha eneo la mradi.

Vile vile alisema kuwa kuna hatari kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kukumbwa na harufu kali kutokana na wakazi wanaoishi karibu na barabara kujiunganishia kinyemela mabomba ya maji machafu na mifereji ya mvua.

Magufuli aliagiza watu wote wanaokwamisha mradi huo kuchukuliwa hatua kali, ikiwa ni pamoja na halmashauri kuwajibika katika hilo.


MTANZANIA

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO- 2013

 
 Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai. 


Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika. 


Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo. 


Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa baada ya kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa Halmashuri/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa.

 (Wizara haitabadilisha shule walizopangwa wanafunzi)

Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:
   Original Result slip na Living Cerificate


PHILIPO A. MULUGO (MB)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10 Julai, 2013WASICHANA....<<<  BOFYA  HAPA>>


WAVULANA....<< BOFYA  HAPA>>> 

 >>Ukitaka  kuya  download  bofya  hapo chini

WASICHANA:  << DOWNLOAD>>

WAVULANA:  << DOWNLOAD>>

MWANACHUO WA MWAKA WA KWANZA ALAANI KITENDO CHA KUPIGWA "EXILE" NA MADENTI WENZIE


Vitendo  vya  wanafunzi  kupigana  exile( kumpisha room ili angonoke na mpenzi wake)   vimekuwa  vikishika  kasi  ya  ajabu  katika  hosteli  za  wanafunzi  wa  vyuo  vikuu  mbalimbali ambao  kwao  limekuwa  ni  jambo  la  kawaida...!!

Hali  imekuwa  ni tofauti  kidogo  kwa  mwanafunzi  wa  chuo kimoja  hapa  nchini  ambaye  yuko  mwaka  wa  kwanza na anategemea kuingia mwaka wa pili.


Akiongea  na  mtandao  huu  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina , mwanafunzi  huyo  amefunguka  na kudai  kuwa  Exile  imemuathiri  sana  kisaikolojia.Imemfanya  aishi  kama  mtumwa  huku  taaluma  yake  ikiyumba  kwa  kasi.

Hili  ni   simulizi  la  mwanafunzi  huyo:
 
"Maisha ya shule yana changamoto  nyingi sana.Kwa  mtu  yeyote  ambaye  ni  mcha  mungu  ni  lazima  itamuwia  vigumu  sana  kukabiliana  na  hali hii.

"Nasema  hivi  kwa  sababu  ndani  ya  hosteli  huwa  tunaishi  watu   tofauti  wenye malezi  tofauti.Kasheshe  ni  kwetu  sisi  first  year...

"Mazingira  kwetu  ni  mageni  na  ndani  ya  hosteli  tunaishi  na  mabraza  wa  miaka  ya  juu  wenye  wapenzi  wao  hapo hapo chuoni ambao  huwaleta  vyumbani   na  wakati mwngine  hulala  nao.

"Wanapokuja  na  wapenzi  wao  vyumbani  ni  lazima  uwapishe  wafanye  mambo  yao.Na  ukiwapisha  maana  yake  utoke  kwa  zaidi  ya  masaa  matatu  mpaka   matano

"Ndani  ya  chumba  changu  tulikuwa  tunaishi  watatu, mmoja  mwaka  wa  pili, mwingine  wa  tatu  na  mimi  mwaka wa kwanza.Wote  hao  walikuwa  na  wapenzi  wao  hapo hapo  chuoni.

"Siku  zote  za  wikiendi  walikuwa  wamezigawana.Mmmoja  ilikuwa  ni  jumamosi  na  mwingine  jumapili.Yaani  kwa  kifupi  ni  kwamba  sikuwa  na  uhuru wa  kukaa  chumbani   siku za wikiendi  na  wakati  mwingine  hata  siku  za  wiki.

"Nimeamua  niwe  muwazi  maana hali  hii  imekuwa  ni  kero  kwangu   na  imekuwa  ikiniathiri  sana  kisaikilojia  na  kusababisha  taaluma  yangu  iyumbe  nikilinganisha  na  nilipokuwa  naanza.

"Naomba  nitoe  ombi  kwa  wanafunzi wenzangu.Sote  tuko  vyuoni  kutafuta  maisha  na  zile  hosteli  tunazilipia  kwa  gharama  sawa.Kwa  nini  umsumbue  mwenzako  wakati  gesti  zipo?..Yangu  ni  hayo  tu"

HUYO NDO "MELLIS EDWARD" ALIYEKAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA AKIWA NA "AGNESS MASOGANGE


Picha  ya  Mrembo Mellis Edward  aliyedakwa  na  madawa  ya  kulevya  Afrika  kusini  akiwa  na  Agness Masogange
Mellis Edward
Inahisiwa kuwa  huyu mwanamke wa pili aliyetajwa na Kamanda Nzowa kwa jina la “Melisa Edward”  ni mdogo wake na Agnes ambaye katika akaunti ya facebook anayo tumia jina la (MELLIS EDWARD) , Agnes amemuweka katika orodha ya family kama ‘sister’ katika akaunti yake ya Facebook.
 Kamanda  Gofrey  Nzowa - Kitengo  cha  Madawa ya Kulevya


 Agness Masogange  akiyahesabu  "MAPESA" yake.Picha  hii aliiweka  siku  chache  zilizopita

"JACK WOLPER ANATAFUTA UMAARUFU KUPITIA JINA LANGU....KAMA SANAA IMEMSHINDA BASI AKAJIUZE AU AKAUZE VIPODOZI"...BABY MADAHAMWIGIZAJI wa kike na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Baby Madaha Joseph amemshukia mwigizaji mwenzake wa kike Jack Wolper kwa kudai kuwa amekuwa akitumia vyombo vya habari kumsema na baadae kujifanya anamuomba msamaha huku hana dhamira ya kweli.

Akiongea na FC , msanii huyo amesema kuwa  Jack  Wolper anatumia jina lake ili apande na kuwa Maarufu (nyota ).

“Mimi ni mwanamke mpigaji na ninajua ninachofanya katika maisha yangu...

"Kuna wanawake hawajui misingi ya sanaa.Ni wanawake ambao  wamevamia fani na kutuharibia  sifa  zetu  kama  wasanii..

"Mimi siwezi kugombana na mtu mwenye fani moja ,tena  ya kubebwa . Jack hana cha kufanya akifeli kuigiza labda arudie kazi yake ya kuuza vipodozi...Atafanya nini kingine hapa mjini zaidi  ya  kujiuza?,”alisema Baby Madaha  na  kuongeza:

“Jack anataka kukiki kwa kunichafulia jina langu, lakini mimi ni Star mwenye vision na najua nafanya nini katika Industry..

"Mimi ni kiongozi mtarajiwa .Nategemewa niongoze watu , sasa nikianza kugombana na watu itaniharibia  ndoto zangu za kisiasa,” 

FC