Dec 27, 2013

"Mkorogo Umenitia Adabu sana"...Wema Sepetu..!!


MISS Tanzania 2006 aliye pia staa wa filamu za Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa, mkorogo umemtia adabu na anajuta kuutumia  mwilini mwake.
Wema Sepetu
Akizungumza juzi na paparazi wetu ofisini kwake jijini Dar, Wema alisema  kuwa baada ya kwenda kliniki nchini China na kupata matatibu ya ngozi yake ambayo sasa imerudi kama mwanzo amejifunza kitu.

NI KITU GANI HICHO?
Wema alisema amejifunza kuwa, binadamu anatakiwa kuishi alivyoumbwa na Mungu, mambo ya rangi ya mwili hayana nafasi katika uwezo wa binadamu.

ALIAMINI USTAA NI LAZIMA UWE MWEUPE PEE!
Wema akatoa mpya zaidi aliposema kuwa, uamuzi wake wa kutumia mkorogo ili awe mweupe kama mzungu (yeye ni mweupe) ulitokana na kuamini kwamba, weupe na ustaa ni mambo yanayokwenda pamoja, kumbe sivyo.

Niliamini weupe sana na ustaa ni Kulwa na Doto, lakini sivyo. Ngozi yangu ya awali ni nzuri, imerudi kama ilivyokuwa, namshukuru sana Mungu,” alisema Wema.

AWAONYA MASTAA WENZAKE
Akiendelea kuzungumza na paparazi, Wema alitoa ujumbe kwa mastaa wenzake wanaotumia mkorogo kuwa, hakuna faida yoyote, kwa sababu mkorogo unaondoa vitamini yote mwilini.

Daktari kule China aliniambia kuwa licha ya kupoteza vitamini nyingi mwilini, pia mkorogo unakufanya mtu uzeeke kabla ya  wakati. Mimi nawaomba kabisa mastaa wenzangu wajiepushe na hii kitu inaitwa mkorogo,” alisema Wema.

ALICHOJIFUNZA KUHUSU KUJIKOBOA
Kujikoboa ni kuwa mweupe sana, lakini Wema anasema alichojifunza kuhusu hali hiyo ni kwamba, ni rahisi sana kuiondoa ngozi ya awali kwa mkorogo lakini inapofika ngozi ya awali inatakiwa kurudi inagharimu sana.

Ukitaka kuona maajabu sasa, ngozi yako mwenyewe kuibadilisha si kazi na wala si gharama lakini ukitaka irudi kama mwanzo ni lazima ugharimike sana, mimi sitaki tena jamani,” alisema Wema.

No comments: