Apr 27, 2013

BAADA YA KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BAYERN, BARCELONA YAJIPANGA KUWANUNUA WACHEZAJI HAWA..

imageimage image  
Sio mara nyingi kwa timu kama Barcelona ikajikuta ikifungwa magoli manne kwenye mechi moja ambapo moja ya mara hizo chache ambazo ulimwengu ulishuhudia ni hii ya juzi kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa ambapo Bayern Munich bila huruma iliwafunga Barca 4-0.
Kipigo hicho ambacho si watu wengi walikitarajia kimewafanya Barcelona kuamka na kuahidi kufanya usajili wa wachezaji watano ili kuimairisha kikosi chake na labda kujaribu kuepuka aibu kama ya juzi ambapo taarifa hii imethibitishwa na makamu wa rais wa Barcelona Josep Bartomeu ambaye amesema kuwa klabu yake ina malengo ya kusajili angalau wachezaji wanne au watano ili kujiimairisha .
Bartomeu amesema kuwa Barca inahiaji kujiimairisha zaidi ili kuendelea kucheza kwenye kiwango cha juu ambapo mwanzoni mwa msimu huu Barca ilisajili wachezaji wawili ambao ni beki Jordi Alba toka Valencia na Alexander Song toka Arsenal huku kukiwa na tetesi zinazosema klabu hiyo tayari imeingia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil Neymar ambaye amesema ataihama klabu yake ya Santos baada ya msimu wa mwaka 2014.
Moja ya wachezaji waliotajwa kuwa kwenye orodha ya kusajiliwa na Barcelona ni beki wa Ujerumani na Borrusia Dortmund Mats Hummels pamoja na beki wa Chelsea David Luiz.

No comments: