Feb 18, 2013

ROSE NDAUKA ‘AKANUSHA’ KUTAPELIKIMYA kingi na stori kibao mtaani juu ya kuingia mitini na ‘mkwanja’ wa  waigizaji  wapya,  hatimaye staa  kutoka  tasnia ya filamu  Bongo, Rose Ndauka kwa  mara nyingine  ameibuka na  kutupilia mbali taarifa  kuwa  amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha kisha  kutokomea kizani  bila kuwashirikisha katika filamu zake.

Akizungumza na  na cloudsfm.co mapema leo  kufuatia uwepo wa  habari kuwa  kuna kundi la wasanii wamefika kwenye  ofisi zake zilipo maeneo ya kinondoni  Jijini Dar kudai fedha  zao  baada ya kushinda usaili uliofanywa na  Rose  na kuambulia  patupu pasipo kushirikishwa katika filamu yoyote ya msanii huyo.

“Sijawahi kuchukua fedha ya mtu na kumnyima nafasi, kinachotokea ni tatizo la wasanii kukosa uvumilivu kwani si rahisi kumchukua kila mtu aliyeshiriki na kushinda usahili na  kumuweka kwenye filamu,   tunachokifanya ni kutoa nafasi moja  kutokana na kipaji halisi kisha wengine wanafuata, lakini ajabu naona wengine wanalalamika bila  kuelewa  lakini sijawahi kula hela ya mtu”  alisema  Rose.

No comments: