Feb 18, 2013

Mbowe aivaa serikali ya CCM

Mbowe aivaa serikali ya CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelaani matukio ya vurugu na mauaji yenye misingi ya tofauti za kidini, huku kikidai ni matunda ya mbegu ya udini na ukabila uliopandikizwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nia ya kuvidhoofisha vyama vya upinzani.

Akifungua kikao cha viongozi wa chama hicho Kanda ya Kaskazini jijini Arusha jana, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliitaka CCM na serikali yake kuhakikisha nchi inakuwa salama.

Alisema CCM kwa kudhani inavikomesha vyama vya upinzani, iliasisi, kueneza na kushabikia sera na chochoko za ubaguzi wa kidini kwa kuwadanganya wananchi kuwa, baadhi ya vyama ni vya kidini na kikabila, matokeo yake sasa udini umeanza kuwa kansa inayoitafuna taifa.

CCM walidhani chokochoko za udini na ukabila zitaviangamiza vyama vya upinzani na kukisaidia kuendelea kusalia madarakani. Hawakujua wanapandikiza mbegu mbaya miongoni mwa Watanzania waliozoea kuishi kwa amani na umoja bila kujali tofauti zao za kidini na kikabila,” alisema.

Mbowe alisema kuwa CCM wamelikoroga, sasa lazima walinywe kwa kuhakikisha taifa linakuwa moja na lenye amani.

Alisema siyo sahihi viongozi wa dini, wawe masheikh, wachungaji, mapadri au mtu awaye yote, kushambuliwa, kumwagiwa tindikali wala kuuawa katika matukio yenye hisia na sura za kidini.

Mbowe alisema ni jukumu na wajibu wa serikali kuwahakikishia raia wake usalama wa maisha na mali zao.

Alisema chama chake kinaamini katika misingi ya taifa lenye haki, amani, umoja na mshikamano kwa watu wote bila kujali tofauti za kidini na kikabila.

Mbowe alisema misingi ya watu makabila yote hapa nchini wa imani tofauti za kidini, ya kuishi kwa kuheshimiana na kushirikiana, lazima ilindwe na kuendelezwa kwa kila mtu kutekeleza jukumu lake la kuenzi tunu hiyo iliyoasisiwa na kupiganiwa na waasisi wa taifa.

Katika vipindi tofauti, viongozi wa CCM na serikali yake walikaririwa wakitangaza kuwa Chama cha Wananchi (CUF) na CHADEMA vina misingi ya kidini na kikabila kama moja ya mbinu za propaganda.

No comments: