Feb 18, 2013

JIBU ALILOLITOA NAPE NNAUYE KUHUSU KAULI YA CHADEMA


.
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kimesema kwamba uchaguzi mkuu wa CCM uliomalizika hivi karibuni ulitawaliwa na rushwa ambayo ilisababisha malalamiko ya matumizi makubwa ya fedha wakati wa uchaguzi.
Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA Mabere Marando amesema kundi kubwa la walioshinda kwenye huo uchaguzi halina uwezo kuanzia wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC), wenyeviti pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya mkoa, wilaya, kata na vijiji.
Marando amesema hiyo ishu itasababisha CCM ipate wakati mgumu katika chaguzi zijazo, namkariri akisema “matukio ya rushwa na ufisadi yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu huo, kuna viongozi waandamizi wa CCM ambao wamelalamika hadharani kuhusu kuenguliwa kutokana na rushwa ndani ya CCM, walijidai kwamba hatua zitachukuliwa dhidi ya vitendo hivi na wahusika lakini mpaka leo uchaguzi umekwisha tunajua hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya mtu yeyote”
Nape Nnauye.
Baada ya hii kauli, jibu la aliyoyasema Marando lilitolewa na katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye ambae naanza kwa kumkariri akisema “kwanza inashangaza kwamba pilipili usiyoila inakuwashia nini, sijaelewa nini kilichomuwasha mzee wangu ninae muheshimu Mzee Mabere Marando kutoa kauli kama hiyo, kama CHADEMA wangesifia timu tuliyoiweka ingebidi twende kuipangua kwa sababu tungekua tumekosea sana, ukiwa na mtu unashindana nae alafu akwambie umeweka kikosi kizuri cha kushindana nae ujue hicho kikosi hakina uwezo wa kumshinda unaeshindana nae”
Kwenye sentensi nyingine, Nape amesema “yeye sio wa kwanza, alianza Babu Dr. Slaa akasema Oooh unajua timu ni ile ile, kama yapo maeneo yalikua na malalamiko ya rushwa tumekamilisha juzi, kamati na udhibiti na nidhamu itapitia maeneo machache ambayo yamelalamikiwa”

No comments: