Mchungaji Odoroti Gunda akitoa hotuba kwa niaba ya Askofu Andrew Gule
Waimbaji wa nyimbo za Injili nchini wametakiwa kujitambua na kufahamau kuwa wana nafasi kubwa ya kutumia vipaji vyao walivyopewa na Mungu kukemea maovu yanayotendeka kwenye jamii na kuilemisha jamii hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Askofu Andrew Gule wa KKKT Dayosisi ya mashariki ya ziwa Victoria katika uzinduzi wa mkanda wa video ya Kwaya ya KKKT Msamalia ya Nyasubi Mchungaji Odoroti Gunda amesema kuwa waimbaji wana uwezo mkubwa wa kuifundisha jamii kupitia nyimbo za Injili ili kukemea maovu yanayotekea nchin hususan mauaji ya vikongwe mkoa wa Shinyanga.
Aidha Gunda amewataka waimbaji kuwa na ushirikiano mzuri ambao utaleta tija kwa jamii na kwaya hiyo kwa ujumla.
Kwa upande wake mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya Solomon Mukubwa ameushukuru uongozi wa Kwaya ya KKKT msamalia kwa kumpa mwaliko wa kuja kuungana nao katika uzinduzi huo na amehaidi kutoa ushirikiano katika jitahada za kuitangaza kwaya hiyo katika nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili toka Kenya Solomon Mkubwa.
Meza ya mgeni Rasmi wakifuatilia uzinduzi huo.
Masanja Mkandamizaji ndiye aliyekuwa Mc katika uzinduzi huo.
Solomon Mkubwa akiwa na Masanja mkandamizaji wakiimba wimbo wa Mfalme wa Amani.
Wanakwaya wa KKKT Msamalia wakifurahi waimbo wa Mfalme wa Amani
Masanja na Solomoni wakizidi kuburudisha.
Wananchi wa Kahama waliohudhuria uzinduzi huo.
Wanakwaya wa Msamalia kwaya walipendeza sana.
Katibu mtendaji wa usharika wa Agape Ibrahimu Nyanga akifuatilia kwa makini uzinduzi wa Mkanda huo.
Walipendeza sana wana KKKT Msamalia.
Ukumbi ulipendeza sana kwakweli.
Wanakwaya wa KKKT Msamalia wakiburudika.
Wanakwaya wa KKKT Msamalia wakionyesha ujuzi mbele ya kadamnasi.
Mchungaji Odoroti Gunda akitoa hotuba
Wanakwaya wa Msamalia wakiandaa Cd kwa ajili ya uzinduzi.
Fundi mitambo akiandaa mitambo kwa ajili ya kuonyesha Live Cd hiyo.
Mgeni Rasmi akiibariki Cd kabla ya kuizindua.
No comments:
Post a Comment