Aug 15, 2012

ABEL KAHOLWE: AJITOSA KWENYE SIASA NA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UENYEKETI WA UVCCM MKOA WA SHINYANGA.


ABEL KAHOLWE MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA  WA SHINYANGA.
Jina lake anaitwa Abel Kaholwe ni kijana mwenye umri wa miaka 24,kijana mwenye ndoto za kufanikisha malengo ya vijana wa shinyanga na tanzania kwa ujumla kupitia vijana wenyewe.
Amechukua maamuzi ya kuomba nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM MKOA WA SHINYANGA ili kufanikisha mambo yafuatayo;
Nilikutana naye katika lango la ofisi ya CCM mkoani Shinyanga akirejesha fomu yake,Nilipata shauku ya kujua machache kuhusu yeye,Na hasa nilitaka kujua ataufanyia nini mkoa wa Shinyanga kama atashika hatamu ya nafasi ya UVCCM  mkoani hapa.
Naye alisema haya,
1.Kufikia malengo na shauku ya vijana kwa kutumika kama sauti yao katika vikao nyeti vya CCM ngazi ya mkoa na taifa ili kuwezesha mabadiliko yenye kufuata matakwa ya vijana katika sera,sheria na utekelezaji wa shughuli za serlikali.
2.Kutumia elimu yake na uzoefu wowote alionao ili kufanikisha mikakati ya maendeleo ya jumuiya,maamuzi ya mikakati yote yatatokana na vikao na mikutano ya kikatiba.
3.Kusimamia rasilimali za jumuiya ya vijana ili ziwe na tija katika maendeleo ya vijana wenyewe.
4.kushirikiana na viongozi wengine na watendaji wa jumuiya na zinazosimamiwa na CCM PAMOJA NA VIONGOZI NA watendaji wa CCM KATIKA NGAZI ZOTE ili kuwajengea uwezo na kuwawezesha vijana kukabiliana na changamoto za kimaisha na kupanga maendeleo ya pamoja huku wakishiriki kikamilifu utekelezaji wa ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.
5.Kuhakikisha ushindi kwa CCM katika chaguzi zote kubwa na ndogo katika mkoa wa shinyanga na tanzania kwa ujumla.

HAYA NI BAADHI TU YA MAMBO MEMGI ANATAKAYOYAFANYA BAADA YA KUPATIWA RIDHAA YA KUWATUMIKIA VIJANA  
PAMOJA TUNAWEZA FIKIA MALENGO YETU KAMA TUTAKUWA NA MATUMAINI NA TUTATAFUTA NA KUTENGENEZA FURSA KADRI INAVYOWEZEKANA.
PAMOJA TUNAWEZA,VIJANA NI TAIFA LA LEO NA KESHO

No comments: