Aug 13, 2012

BREAKING NEWS: DREVA BODABODA ASABABISHA AJALI YA BASI LA LEINA TOUR LAUA MWANAMKE MMOJA KAHAMA.


Basi la Leina Tour mara baada ya kupata ajali

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Happy John(37) mkazi wa Tarime mkoani Mara amekufa na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa kufuatia ajali ya Basi la Kampuni ya Leina Tours kupinduka katika barabara ya Isaka mjini Kahama.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Evalist Mangala amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 asubuhi wakati basi hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T391 BWP lilokuwa likiendeshwa na Dreva aliyefahamika kwa jina la moja la Hamisi  mkazi wa Dar es salaam kuacha njia na kupinduka wakati akijalibu kumkwepa dreva pikipiki.

Amemtaja dreva wa pikipiki kuwa ni Willson Paschal (24) mkazi wa Nyahanaga ambaye amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama akipatiwa matibabu.

Kwa muijbu wa kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Kahama Dr Fredy Endrue amesema amepokea majeruhi 42 ambapo kati yao Majeruhi 15 wakiwemo raia 3 wa nchi ya Rwanda na Kongo wametibiwa na kuruhusiwa,Majeruhi waliolazwa ni 27 ambapo kati yao 10 ni raia wa kongo na Rwanda. 

Aidha amesema kuwa majeruhi wawili ambaye ni Kayumba Yusuph (52) mkazi wa Dar es salaam na Willson Paschal (24) mkazi wa Nyahanga Kahama hali zao ni mbaya na wanaendelea na matibabu,

Jeshi la Polisi wilayani Kahama linaendelea kumtafuta dreva wa basi hilo ambaye amekimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea na uchunguzi zaidi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea.

 
Polisi wa usalama barabarani wakipima eneo la ajali.

 
Mwonekano wa basi la Leina Tour kwa chini.
 
Wafanyakazi wa kampuni ya Leina Tours wakijadiliana jambo.

Jeshi la Polisi wakihamisha mizigo ya abiria kuipeleka kituoni kwa usalama zaidi
Taratibu basi linainuliwa 

Basi la Leina Tours mara baada ya kuinuliwa.

Jeshi la Polisi likihakikisha ulinzi mara baada ya kuinuliwa kwa basi hilo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimdhibiti kijana ambaye alitaka kusogelea eneo la ajali.

Wananchi wa Kahama wakiliangalia basi la Leina mara baada ya kuinuliwa.
 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh Mpesya akiwa katika wodi ya wanaume ya Hospitali ya wilaya ya Kahama akiwasalimia majeruhi.

Mmoja wa majeruhi akimwonesha jeraha mkuu wa wilya ya Kahama.

Mh Benson Mpesya kulia akizungumza na  Dr Kangombe.

Mh Mpesya akimuangalia Dreva pikipiki Willson Paschal ambaye ndiye aliyekuwa anakwepwa nabasi hilo

Wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Kahama wakishirikiana kuokoa maisha ya Willson Paschal amabaye ni dreva pikipiki.

Dreva pikipiki Willson Paschal akipatiwa matibabu

No comments: