
Majaji wa shindano hilo la B-12 ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 jijini Dar es Salaam akiwa na muandaaji wa kipindi cha ‘Step Up Player’ Isakwisa Thomson wakijaribu kumnyamazisha Msami kutoka T.H.T ambaye alianza kulia kabla ya kutangaza matokeo jambo ambalo lilionyesha ni jinsi gani asivyopenda watu washinde kufanya vyema.

Mc wa shindano hilo Babuu wa Kitaa ambaye ni mtangazaji wa Clouds Tv akiongea na wanaikundi cha Underzone baada ya kumaliza kuonyesha umahili wao.

Hakika ilikuwa ni vuta nikuvute maana kila kundi lilionyesha umahili wa ucheza na muonekano wa mavazi pia.

UB-40 kutoka Zanzibar nao hawakuwa nyuma kuwasha moto.

Adamu Mchomvu ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm na pia ni msanii wa bongflava anayetamba na nyimbo yake ya John! John! akiwasha moto ndani ya Maisha Club ambapo alisindikiza fainali ya shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2011.
No comments:
Post a Comment