Jun 21, 2011

Ney wa Mitego: Sijaoa ila mademu wananisumbua sana

Inakuwaje watu wangu? Natumaini mko poa kabisa! Wiki hii nawaletea msanii anayefanya vyema kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva anayefahamika sana kwa jina la Ney wa Mitego lakini jina lake kamili alilopewa na wazazi wake ni Emmanuel Elbariki.

Jamaa alizaliwa mwaka 1985 Manzese jijini Dar es Salaam, amegonga elimu ya msingi katika Shule ya Ukombozi na baada ya kuhitimu, alijiunga na kidato cha kwanza katika Sekondari ya Mbezi Beach na kuishia kidato cha nne. Mengi zaidi kuhusiana na msanii huyu ungana nami katika maswali kumi niliyomuuliza.

TQ: Baada ya kuhitimu kidato cha nne ulifanya nini na lini hasa ulijiingiza kwenye muziki?
NAY WA MITEGO: Baada ya kuhitimu kidato cha nne niliendelea na shughuli zangu za kawaida na muziki nikaja kuuanza mwaka 1996. Nilianza kuimba mwenyewe, baadaye nikajiunga na kundi liitwalo Wazee wa kazi ambalo halikudumu kwa muda mrefu ndipo nikaanza kujitegemea.

TQ: Unakumbuka wimbo wako wa kwanza ulitoka mwaka gani na ulijisikiaje uliposikia redioni?
NAY WA MITEGO: Nakumbuka, ulitoka mwaka 1998 ulikwenda kwa jina la ‘Hands up’, nilijisikia furaha sana.

TQ: Kwa hapa Bongo ni msanii gani ambaye ungependa kufanya naye kazi?
NAY WA MITEGO: Ni wengi lakini zaidi nawakubali sana Juma Nature na 20%.

TQ: Je, umeoa, una mchumba au ndiyo wale wale ambao wapo wapo sana?
NAY WA MITEGO: Kusema ukweli sijaoa lakini wapenzi ninao wa kutosha.

TQ: Hii nayo kali, inakuwaje mtu mmoja unakuwa na wapenzi kibao?
NAY WA MITEGO: Imetokea tu na nawamudu kimtindo, si unajua mimi ni mwanamume niliyekamilika?

TQ:Kwa staili hiyo utao kweli?
NAY WA MITEGO:Yes! Naamini kati ya hawa yupo mmoja mwenye mapenzi ya kweli na huyo ndiye atakuwa mke wangu.

TQ: Vipi kuhusu Ukimwi?
NAY WA MITEGO:Niko makini kuliko unavyodhani.

TQ: Hebu tuambie unapokuwa faragha na mpenzi wako ni maneno gani ambayo akikuambia unadata?
NAY WA MITEGO: Huwa napenda anaponiambia asante tukimaliza mambo yetu kwani inaonesha ameridhika na kile nilichompatia.

TQ: Ni changamoto gani unakumbana nazo katika kazi zako za kimuziki?
NAY WA MITEGO: Changamoto ni nyingi ikiwemo kusumbuliwa na mademu, malumbano na wasanii wenzangu kutokana na muziki ninaoufanya kwa sababu naongea ukweli na nyinginezo.

TQ: Penye changamoto na mafanikio yapo, ni mafanikio gani umeyapata mpaka sasa kutokana na kushika ‘mic’?
NAY WA MITEGO: Hakuna mafanikio ya kiviile, kikubwa nayeendesha maisha yangu na nimejuana na watu wengi ambao huenda nisingekuwa msanii nisingejuana nao.

TQ:Nakushukuru Nay, kila la kheri katika mishemishe zako.
NAY WA MITEGO: Asante sana.

No comments: