Apr 25, 2011

LINEX, TOP C, BABA LEVEL, QUICK RAKA NA KAMATA MWIZI MEN WAUA KAHAMA!!!!!!!!!









Moyo wa subira wafunika Kahama. Ni baada ya kijana linex kuzindua album yake inayokwenda kwa jina la Mama Halima. Ngoma ya moyo wa subira ndio ngoma inayo run katika ulimwengu wa mziki wa kizazi kipya tukiwa tunazungumzia mziki wa bongo flava. Katika uzinduzi huo akiwa ameambatana na wakali kibao akiwemo baba level, Kamata mwizi men maarufu kwa jina la Sharobaro, pamoja na kijana Quick raka wakazi wa kahama hawakujutia kulipa kiingilio chao katika ukumbi wa masabo kwani kijana linex aliwakonga mashabiki wa mziki wa kizazi kipya bongo flava, akilitawala vyema jukwaa na kuwafanya wakazi wa kahama kuyahesabu mazuri aliyoyafanya klijana linex. Akifanya mahojiano na lost-9fm kijana linex akiwa marine hotel anasema, mapenzi ndio mpango mzima mambo hayawezi kwenda bila mapenzi. Kijana linex amewasihi wakazi wa kahama wawe na moyo wa subira. Baada ya kushuhudia show hiyo kali ya linex lost-9fm ilifunga safari hadi ukumbi wa Hamilton ambako liliangushwa show kali na ma Djs wa clouds fm pamoja na kijana Top C akiwashika vilivyo wakazi wa mjini kahama na ngoma yake ya Sababu ya ulofa. DJ Masu ndiye aliyekuwa wa kwanza kukaa kwenye one and two akiwapagawisha wakazi wa kahama akifuatiwa na 4 by 4 Dj Elly mzee wa night kali. Dj Masu aliwachanganya mashabiki wa mziki wa kizazi kipya ni baada ya kutoa zawadi kwa kijana aliyekuwa amependeza zaid kuliko wengine kwa zawadi ya sh. 5000, Dada pia aliyekuwa ametoka chicha kuliko wengine lakinin kali zaidi ni pale alipotoa zawadi kwa mwana dafada aliyemiliki jukwaa kwa kucheza kiduku zawadi ya sh 10000. Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti wapenzi wa muziki wa bongo flava wakiwaomba ma Djs wa radio clouds fm wawaletee Fiesta kwani wakazi wa mjini kahama wamesahaulika na suala zima la burudani naye akijibu ombi la wakazi wa kahama kwa niaba ya clouds fm Dj Elly alisema kuwa fiesta intaungurumishwa ndani ya uwanja wa Taifa mjini kahama bila wasi wasi wowote jibu hilo liliitikiwa kwa furaha kubwa. Lost-9fm ilifunguka kutoka disco mishale ya saa kumi na moja na nusu alfajiri kurudi masikani. ( PICHA NA DJ LAZZER5IVE)

3 comments:

dj lazzer5ive said...

Kijana linex ni noma aise mtoto anaimba ile mbaya huchoki kumsikiliza. kitu moyo wa subira ni nomaaaaaaaaaa. keep it up men

dj lazzer5ive said...

baba nilipitwa kinoma nasikia dogo linex kapoteza mbaya mbovu

Unknown said...

kijana unatisha kama vp big up kaka, endelea ku2pa mambo