Jun 13, 2013

Vitendo vya Ushoga vyazidi Kuongezeka Bongo Hawa Tena Washikwa Gesti Wakibanjuana




Tukio hilo lililoshuhudiwa na watu kibao, lilijiri Juni 10, mwaka huu katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Kunaswa kwa wanaume hao ambao ilidaiwa walikuwa kwenye harakati za kufanya Usodoma na Ugomora, kulifuatia mke wa mmoja wao kunasa meseji za kimapenzi walizokuwa wakitumiana wawili hao.

Mama huyo alipobaini meseji hizo chafu, wawili hao wakisisitiziana kukutana kwenye gesti hiyo usiku wa siku hiyo, alimpigia simu mmoja wa waandishi na  kumpa  mkasa  mzima ambapo  walikubaliana  saa  moja  zoezi  la  kuwanasa  litaanza..

Ilipofika saa 1:30 usiku, timu yetu, mama huyo, wapambe wake na polisi walikuwa wanafanya doria nje ya gesti hiyo.


Saa 5:30 usiku, mume wa mwanamke huyo akiwa na mwanaume anayedaiwa kuwa shoga walifika gesti hiyo bila kujua kama waliwekewa mtego wa kunaswa na kwenda kuchukua chumba namba 2.
 Wakiwa ndani, mke alimpigia simu mumewe na kuhoji alipokuwa akajibiwa alikuwa mitaa ya nyumbani kwao Manseze, Dar akipiga stori na rafiki zake.

Wawili hao wakiwa wanajiandaa na mchezo wao usiofaa, polisi aligonga mlango akijifanya mhudumu aliyetaka kumpatia taulo, jamaa bila kujua alifungua ndipo walipofumaniwa na kuibua varangati zito.

Kufuatia timbwili hilo, waliwekwa chini ya ulinzi na kutolewa pale gesti tayari kupelekwa kituoni ndipo mwanaume anayedaiwa kuwa shoga akatimua mbio mithili ya mwanariadha wa kimataifa, Usain Bolt wa Jamaika na wanandoa hao waliendelea kuzozana huku mke akimlalamikia mumewe na kumwambia wakifika nyumbani ampe talaka yake.


Hata hivyo, mwanamke huyo aliomba sakata hilo lisipelekwe polisi kwa madai alichotaka ni kumfumania mumewe na kwamba alikuwa na ushahidi wote.

No comments: