Jun 13, 2013

BAADA YA VIFO VINGI, WASANII WAHAMASISHANA KUMRUDIA MUNGU


KUTOKANA na vifo vya mara kwa mara vya wasanii, staa wa filamu za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema ni wakati wa wasanii kumrudia Mungu.

Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Dude alisema kwa kipindi kifupi vimetokea vifo vingi vya wasanii tena wenye umri mdogo, hivyo anawataka wasanii wabadili mfumo wao wa maisha kwa kuachana na mambo maovu, anasa za dunia kwani hawajui siku wala saa ya kufariki dunia.
 

“Wasanii tunazidi kufa, juzi tumemzika Ngwea, leo tena Kashi wasanii tunatakiwa kufanya ibada, wenye sauti za kuimba wamwimbie Mungu kwani waliotangulia hawakujua kama watakufa, binafsi nimeanza kusali tangu nilipofiwa na mama yangu,” alisema Dude.

No comments: