SPACIO ABUBAKARI
Kwa jina naitwa Spacio Abubakary Ngalla, nimezaliwa na
kukulia Dar es salaam, Sinza. Na ni mtoto wa 3 katika familia ya kiislamu.
Kiukweli mimi nilikuwa mmoja wa watu ambao hawakutaka kusikia
Jina la YESU na nilikuwa siamini miujiza yeyote na kuona ni mazingaombo tu
wachungaji wanafanya kuwateka watu akili. Ila hadi siku ambayo mungu
aliponionesha njia ya uzima na kuniponya tatizo lililonisumbua mda mrefu, ndipo
nikaamini uwepo wa UKRISTO
NILIVYOKUTANA NA JINI MAHABA
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1996, nikiwa na miaka 7, Mimi na
marafiki zangu tulikuwa na tabia ya kwenda kuogelea coco beach siku za weekend,
siku moja baada ya kumaliza kazi zangu za nyumbani majira ya saa 6 hivi
nikaenda kuwapitia marafiki zangu (4) ili twende beach kuogelea ikifika jioni
turudi nyumbani. Tulipofika beach watu walikuwa ni wengi sana kila mmoja
alikuwa yupo busy na yake, sisi tulijigawa wengine walienda kuogelea sehemu
nyingine, mimi na mwenzangu Ali tulibaki upande wa mwanzoni kwa kuwa hatukuwa
tunajua kuogelea vizuri.
Majira ya saa 10, hivi nikiwa na Ali, nilisikia harufu nzuri
kweli ikiwa inavuma kuja kwetu, ambayo siku wahi kuisikia kabla, ni nzuri kwa
kweli, nikamuuliza Ali “unaisikia harufu hii?” yeye akajibu ndio ninaisikia ila
sijui inatoka wapi!
Baada ya dakika kadhaa nilisikia sauti ya kike ikinisalimia
“hujambo?” nikashtuka, kugeuka nyuma nikakutana na msichana sijui nimuelezeeje,
ni mweupe kiasi, ana nywele ndefu, sura yake ipo serious na ukiiangalia tena ni
kama anatabasamu, macho yake ni ang’avu, ni mzuri kiufupi akiwa amevaa nguo za
kawaida tu ila kichwani amejitanda baibui. Aliniambia jina anaitwa MAIMUNA!
Mwili uninisisimka huku kidogo nikiwa na natetemeka japo
sikutaka kumuonesha kwa kuwa hilo jina halikuwa geni kwangu, cha ajabu kadri
alivyokuwa anaongea na mimi uoga ulizidi kunipungua hadi nikawa najiskia kawada
na kucheka pamoja. Aliomba tuogelee wote nikamwambia, mimi siwezi kuogolea
vizuri, akaniambia “Usiwe na wasi wasi nitakufundisha usijali” basi akaanza
kunishika mikono na kuanza kunivuta ili niweze kujifunza kupiga mbizi taratibu.
Siku hiyo ilikuwa ni tofauti sana kwani tulifurahi sana.
Saa 12 na nusu jioni ilipofika tukaanza kujiandaa kwa
safari, siku hiyo tulichelewa kweli kuondoka! Ghafla Maimuna nikawa simuoni,
nikaita sana “Maimunaaaaa uko wapi sisi tunataka kuondokaaaaa!” Kimyaa!
Basi sisi tukaanza kuondoka pale beach,
kuna sehemu huwa ina miti mingi sana na ni shortcut kwenda kituoni, kwa mchana
ni salama lakini kama ni giza giza si pazuri huwa kunakuwa na wahuni. Sisi
tukiwa tunakaribia hiyo njia roho ilisita kupita pale, kumbe nyuma kulikua na
wahuni wakitufatilia. Na sisi tupo watato tu, wao walikuwa watatu.
Heee mara tukashangaa kundi la watu zaidi ya 15 nao wakawa
wanapita hiyo hiyo njia, basi sisi tukaongozana nao hadi kupita ile njia
salama, kushtuka tunajiona tupo wa tano tu mbele tunakajiuliza “wale watu
wameenda wapi?” Wahuni kumbe walikimbia katikati! sasa hatukujua ni kwa kwa
sababu gani. Ila mimi nikahisi kundi la watu wale hawakuwa watu bali ni majini
ndo waliotusindikiza, nikawaambia wenzangu “jamani tukimbie wale ni majini” kwa
sauti kubwa ya uoga”.
URAFIKI NA JINI MAIMUNA
Tukafika nyumbani kila mmoja hoi, mimi bado nilikuwa na
mawazo ya yule msichana niliyekutana nae baharini. Usiku nikiwa ndotoni
nilimuota akija kunitembelea nyumbani na kufurahi pamoja.
Hali ile iliendelea hadi nafika form 1, ambapo nilikuwa
nasoma Azania Sec School, haipiti siku moja lazima niote tuko pamoja tunafurahi
pamoja hadi nikazoea,
Mwaka 2004, Maimuna alijitokeza tena kwa mara ya pili nikiwa
niko chumbani, niliogopa sana nilipiga kelele mama akaja Maimuna akaondoka.
Mama alishushwa sana na hali hiyo akaniuliza tatizo ni nini lakini nikamwambia
nilikuwa naota tu, niliogopa kusema kwa kuwa Maimuna aliniambia nisiseme
chochote kuhusu yeye la sisivyo nitakiona cha moto.
Baada ya muda nikazoea, akija tunaongea tu vizuri na kazi
zingine alikuwa ananisaidia kama kutengeneza computer za baba, alikuwa
ananisaidia kama tatizo ni kubwa sana namwita kimoyo moyo anakuja ktk mwili
wangu kisha naanza kutengeneza computer, watu wengi walinishangaa sana uwezo
niliokuwa nao lakini kumbe walikuwa hawajui JINI ndie alikuwa mara nyingi
ananifundisha usiku.
Alinipa hela nyingi tu kiasi kwamba nilikuwa naenda shule
nikiwa elfu 50, laki, ILA ole wangu nitumie na mwanamke au nimnunulie mtu
sigara, pombe, basi hela zote zinapotea na nitahangaika hata shilingi 100
sipati zaidi ya kupewa hela ya shule, na nitahangaika hadi basi.
KAMA kawaida ukisha fikia umri fulani lazima uanze utundu wa
kufatilia wasichana, kuwapa hela au kuwanunulia zawadi hasa katika siku kuu vile
au valentine day, mimi iliponza sana hiyo tabia, kwani niliteseka sana.Kwani
maimuna alikuwa hapendi
Kitu kilichonifanya nitafute wasichana wengine ni kwamba Maimuna
hakuwa anakuja kila wakati, ni mara moja tu kwa siku tena hasa usiku. Na pia
ukiangalia hata nikija kukua yeye anabaki jini na mimi binadamu kwa hiyo si
rahisi kuja kuishi pamoja.
ILA chochote kilichokuwa kibaya kwangu kilichotegeshwa
kichawi hakikuweza kunipata na hata usiku wachawi hawakuweza kunifata fata,
japo mwanzoni nilihangaika sana na wachawi kwani walikuwa wanatusumbua sana
nyumbani, waganga walidai nyumba haikuwa na zindiko!
Kiukweli alinifundisha vitu vingi pamoja na uchoraji, utayarishaji
muziki, computer ambavyo hadi sasa vinanisaidia ktk maisha yangu, baada ya
kutoka darasani yeye hunifuata usiku na kunielekeza zaidi. MIAKA YOTE HIYO
TULIISHI KAMA WACHUMBA.Mengine siwezi kuyataja lakini mtakuwa mshaelewa nini
ninamaanisha.
UGOMVI NA JINI KUANZA
Mwaka 2009, nina miaka 20 nikiwa nafanya kazi Cellulant
Tanzania, kuna dada mmoja alikosea namba na kupiga kwangu, alijitambulisha kwa
jina anaiwa UPENDO, mara ndio ukawa mwanzo wa urafiki wetu ambae hadi sasa
tunaishi pamoja tukijipanga kwa ajili ya kufunga ndoa. Nilitokea kumpenda sana
dada huyo japo hatukuwa tumeonana, na hata yeye pia alitokea kupenda kuongea na
mimi mda wote. Maimuna alikuwa hapendi tabia ya mimi kuongea na huyo dada na
mara nyingi alikuwa ananionya sana, ila mimi ilikuwa vigumu mno kukubali kwani
nilikuwa nimshapenda tayari.
Siku moja nikasema hataa lazima nionane na huyu dada, hadi
lini tutaishia kuongea kwa simu tu. Kwa mara ya kwanza kukutana na dada huyo,
usiku wake sikulala! Nilipatwa na homa hadi asubuhi yake sikuweza kwenda kazini
ikabidi nipumzike. Mara mwili unachoma, mara kifua kinanibana, mara kichwa
kinaniuma, kikitulia nyama za mwili zinatikisika kama mtu anani vibrate vile.Niliteseka
sana wiki nzima nilkuwa mgonjwa. Maimuna akaniambia hiyo ni bakora moja
nimekupa, nataka uachane na UPENDO.
Baada ya kuseka sana kwa hali hiyo kwani mara kwa mara
ilikuwa inanitokea, nikaanza kwenda kwa waganga kutafuta tiba ya kumuondoa jini
huyo katika mwili wangu,kwani alikuwa kero kwangu, zaidi ya waganga 15
nilikwenda lakini bila mafanikio.
KUOKOKA KWANGU
Baada ya kuchoka kuvumilia nikamfuata rafiki yangu wa karibu
Robert na kuanza kumueleza, akaniambia
kwanini usiende kuombewa, mbona wengi tu wanapona na hata mjomba wangu alikuwa
anaumwa miguu alipoombea akapona. Nikamwambia sasa nikienda huko wazazi wangu
waanifikiriaje? Akanijaza moyo na kunipa ujarisi kuwa “IMANI YAKO NA MUNGU SI
YA WAZAZI WAKO BALI NI WEWE NA MUNGU WAKO NA HATA UKIFA UTAENDA NAO? SI WEWE
NDIE UTAKAYE ENDA KUJIBU HUKO? FANYA MAAMUZI YALIYO SAHIHI”
Nikakubali! Basi nikasubiri jumapili ilipofika nikajiandaa
na kwenda kanisani kuombewa, hakika nilipoombewa kila kitu kili badilika na
kijisikia mwepesi kama vile nilikuwa nimebeba viroba vya michanga! Nilipoombewa
nikadondoka chini na kupoteza fahamu. Baada ya dakika kadhaa nikaamka na
kujikuta nikochini nimelala huku nikijishangaa nini kilichotokea.
Toka hapo nikaamini na nikaamua kuimba Nyimbo za Injili ili
kueneza Neno la Mungu kwa wasiofahamu utamu wake.
Kwasasa nipo huru na ni kweli Yesu anatenda na Roho Mtakatifu
yupo kwa ajili yako endapo utaamua kumpokea! Mungu ni mwema, Mungu anatenda. NAMSHUKURU
KWA KUNIOKOA!
No comments:
Post a Comment