Hivi karibuni tuliandika habari kuhusu kundi linaloundwa na vijana
wanne wenye vipaji kutoka Kenya linalofahamika kama Camp Mulla kumpoteza
member mmoja ambaye ndio aliyekuwa msichana pekee katika kundi aitwaye
Miss Karun.
Mwanzo ulianza kama uvumi kuwa Miss Karun amepigwa chini na kundi
hilo na nafasi yake kuchukuliwa na msichana mwingine aitwaye Tiri,
lakini habari mpya habari zilizothibitishwa Kupitia mtandao wa kituo
kikubwa Africa Kusini Channel O, zinasema Miss Karun ameamua kujiondoa
kwenye kundi kwaajili ya maandalizi ya kujiunga na chuo.
Miss Karun anategemewa kwenda masomoni nchini Marekani mwezi August mwaka huu, lakini ataendelea kufanya muziki kama solo.
Kama vile haitoshi, kwa mujibu wa mtandao huo member mwingine aitwaye
Thee Mc Africa zamani alifahamika kama Taio Tripper naye amejitoa
katika kundi hilo na ataendelea kufanya muziki kama solo.
Kundi hilo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa na members wanne, Kwa sasa
limebaki na members wawili wa mwanzo pamoja na msanii mpya wa kike
aitwaye Tiri.
No comments:
Post a Comment