Apr 23, 2013

"SPIKA WA BUNGE ANALIONGOZA BUNGE KWA " REMOTE CONTROL" TOKA NJE.....HII NI KAULI YA DR. SLAAKatibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amesema Spika wa Bunge Anne Makinda amekinajisi kiti cha spika.

Dr Slaa ambaye ni gwiji wa siasa za Tanzania amemshutumu vikali Spika na Naibu wake kwa kuharibu kabisa bunge la Tanzania na kupoteza kabisa heshima yake ndani na nje ya nchi.


Dr Slaa amefichua kwamba maamuzi yote yanayofanywa na Anne Makinda si kwa utashi wake bali ni kutokana na maelekezo maalum anayoelekezwa kutoka nje ya bunge.


Kutokana na vitendo vinavyofanywa na kiti cha Spika imefika mahali Spika na Naibu wake wanadharauliwa hata na watoto wadogo.


Spika Anne Makinda kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri kuu ya CCM.


Source:ITV Habari.

No comments: