Apr 21, 2013

LUIS SUAREZ AOMBA MSAMAHA KWA KUMNG'ATA IVANOVIC - LAKINI HII SIO MARA YAKE YA KWANZA KUMNG'ATA MCHEZAJI


Luis Suarez ameomba radhi kwa kitendo cha kumng'ata mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic katika mchezo wa leo wa ligi kuu ya premier league kati ya Chelsea na Liverpool ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.
Lakini pamoja na kuomba msamaha huo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kumbukumbu zinaonyesha kwamba hii haikuwa mara ya kwanza kwa Suarez kumng'ata mchezaji mwenzie uwanjani - wakati akiichezea Ajax alimng'ata mchezaji Otman Bakkal  wa PSVkama video inavyoonesha hapo chini.

Baada ya kutokea kitendo hicho leo hii vyombo vya habari vya Uingereza vimekuwa vikisema sasa ni muda muafaka kwa Suarez kuondolewa kwenye ligi kuu ya England kwa kulitia aibu soka la nchi hiyo.

Ajax walimuuza Suarez mara baada ya mchezo huo, ukawa ndio mchezo wake wa mwisho kuitumikia klabu hiyo ya Uholanzi - Je Liverpool nao watafuata ushauri wa vyombo vya habari vya England na kumuuza Mruguay huyo? 
 

No comments: