Apr 7, 2013

EXCLUSIVE: GIGGS, FERDINAND KUTUA BONGO HIVI KARIBUNI...

Ryan Giggs.
Rio Ferdinand.

MMOJA wa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Manchester United anatarajia kutua nchini hapa, Mei mwaka huu ikiwa mipango itaenda kama inavyopangwa.
Championi Ijumaa limefahamishwa juu ya ujio wa wachezaji hao ambapo kwa asilimia kubwa wanaoweza kuja nchini ni Rio Ferdinand au Ryan Giggs.
Mtoa habari wetu kutoka jijini London, England amesema kila kitu kinaenda vizuri.
“Tumeshazungumza na mawakala wa wachezaji hao na wote wameonyesha kuwa tayari, wakatupa masharti yao ambayo siyo magumu kutekelezeka, tulichofanya tumezungumza na kampuni ya simu iliyopo huko Tanzania kwa ajili ya kuratibu mchakato huo.
“Wametuambia watatupatia jibu wiki ijayo, lakini hata kama wakikataa ofa hiyo, kuna kampuni nyingine ambayo imeshaonyesha nia na inachosubiri ni hao wenye kampuni ya simu waseme hawawezi ili wao waichukue.
“Wanakuja kufanya programu za kuwainua vijana na kutangaza utalii na biashara za kampuni mbalimbali, mara ya mwisho tulizungumza na wakala wa Rio tulipokuwa kwenye Uwanja wa Old Trafford hivi karibuni.
“Wakala wa Rio alitaka dola 190,000 (Sh milioni 304) kama malipo ya ujio wa mchezaji huyo, tiketi tano za daraja la kwanza, akataja na hoteli kabisa ya Serena kuwa ndiyo angependa wafikie hapo.
“Lakini pia kuna mpango mwingine unaohusu Arsene Wenger, bado haujakaa sawa na ni mapema kuuzungumzia, nao ukikaa sawa tutawajulisha nini kitakachofanyika juu ya kocha huyo wa Arsenal,” kilieleza chanzo.

CRDTS: GPL

No comments: