Feb 19, 2013

MTOTO HUYU ANAHITAJI MSAADA WAKO


Jina la mtoto anaitwa  Ombeni Mbeula
Mama wa mtosto anaitwa Kilaudia Kigaila
Nyumba iliungua wakati watoto hao wamekaa ndani na wakati huo huo mama wa mtoto alikuwa amekwenda shambani maeneo ya Chitemo iliyoko wilaya ya mpwapwa
Wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba. Baada ya tukio hilo kutokea   ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha   kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa  na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu  haikuweza kupatikana paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya  ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336

No comments: