Aug 14, 2011

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ELEKEZI ZA MAFUTA KUANZIA KESHO AGOSTI 15, 2011



Meneja Biashara wa Mafuta ya petroli kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza na wanahabari jana jijini, Dar es Salaam kuhusu kupanda kwa bei za mafuta. Kulia ni Ofisa Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo. Picha na Richard Mwaikenda.
Kama ilivyo ada, na kulingana na Kanuni ya Kukokotoa bei za bidhaa za mafuta ya petroli bei zimekuwa zikikokotolewa na kutangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kila baada ya wiki mbili. EWURA inatangaza bei elekezi/kikomo za mafuta ya petroli nchini zitakazoanza kutumika kuanzia Jumatatu, Tarehe 15 Agosti 2011. Bei hizi zimekokotolewa kwa kuzingatia kanuni mpya iliyoanza kutumika mwanzoni mwa mwezi huu. Pamoja na kutambua bei elekezi/kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
(a) Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimepanda ikilinganishwa na bei zilizokokotolewa kwa ajili ya kuanza kutumika tarehe 1 Agosti 2011 ambazo zilitangazwa tarehe 3 Agosti 2011. Katika toleo hili bei zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 100.34 sawa na asilimia 5.51, Dizeli TZS 120.47, sawa na asilimia 6.30 na Mafuta ya taa TZS 100.87, sawa na asilimia 5.30. Mabadiliko haya ya bei za mafuta nchini yametokana na kupanda sana kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia). 

Kwa mfano, kwa viwango vya bei zilizotumika katika chapisho hili, bei katika soko la dunia zimepanda kwa wastani wa asilimia 5.42 na thamani ya shillingi ya Tanzania imeshuka kwa shilingi 47.12 (asilimia 2.96) kwa dola moja ya Marekani. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 110.34 sawa na asilimia 5.70; Dizeli TZS 120.47 sawa na asilimia 6.54; na Mafuta ya Taa TZS 100.87 sawa na asilimia 5.49.
(b) Bei za rejareja na za jumla zingepanda zaidi endapo formula ya zamani ingeendelea kutumika. Kwa kulinganisha vigezo vilivyo katika fomula ya zamani na fomula mpya, bei za mafuta zingekuwa kama ifuatavyo:

Aina ya Mafuta
Bei za Rejareja (TZS/L)
Bei za Jumla (TZS/L)
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Petroli
2,298.33
2,114.12
2,230.07
2,046.62
Dizeli
2,213.36
2,031.31
2,140.80
1,963.81
Mafuta ya Taa
2,188.89
2,005.40
2,116.33
1,937.90
Kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo juu, formula mpya inaendelea kutoa unafuu kwa watumiaji ukilinganishwa na kama fomula ya zamani ingetumika. Ni dhahiri kuwa vigezo viwili vikubwa vinavyochochea kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta nchini ni kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dola ya Marekani, sarafu ambayo inatumika kuagizia mafuta hayo.

(c) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(d) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 5 la tarehe 9 Januari 2009 na marekebisho yaliyofanywa mwezi Julai 2011.

(e) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.

(f) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.
A: BEI ZA REJAREJA
Bei Elekezi
Mji
Petroli
Mafuta ya Taa
Dizeli

(TZS/LT)
(TZS/LT)
(TZS/LT)
Dar es Salaam
2,114
2,005
2031
Arusha
2,198
2,089
2115
Arumeru
2,198
2,089
2115
Karatu
2,216
2,108
2133
Monduli
2,203
2,095
2121
Ngorongoro (Loliondo)
2,275
2,166
2192
Kibaha
2,119
2,010
2036
Bagamoyo
2,125
2,016
2042
Kisarawe
2,121
2,013
2038
Mkuranga
2,124
2,015
2041
Rufiji
2,142
2,033
2059
Dodoma
2,173
2,064
2090
Kondoa
2,205
2,096
2122
Kongwa
2,170
2,061
2087
Mpwapwa
2,174
2,065
2091
Iringa
2,178
2,069
2095
Kilolo
2,183
2,074
2100
Ludewa
2,244
2,135
2161
Makete
2,237
2,128
2154
Mufindi
2,188
2,079
2105
Njombe
2,206
2,098
2124
Bukoba
2,329
2,220
2246
Biharamulo
2,303
2,194
2220
Karagwe
2,345
2,236
2262
Muleba
2,320
2,211

Chanzo: Michuzi blog

No comments: