Aug 14, 2011

AJALI YA LORI MORO

Lori aina ya scania lenye namba za usajili, T 440 BBF likiwa na tela lake lenye namba T 228 BBG baada ya kupinduka katika eneo la Kingolwira nje kidogo ya mji wa Morogoro jana usiku.
LORI lililokuwa likisafirisha mzigo wa mbao kutoka Iringa kuelekea jijni Dar es Salaam, jana usiku lilipinduka katika eneo la Kingolwira nje kidogo ya mji wa Morogoro.

Dereva wa lori hilo aina ya scania lenye namba za usajili, T 440 BBF lililokuwa na tela lenye namba T 228 BBG, Bw George Mgeni, alidai kuwa alipatwa na jali hiyo baada ya kujaribu kukwepa lori lingine aina ya fusso.

"Dereva wa fusso awali alikuwa amepaki hapa juu ya mlima nilipomkaribia aliwasha gari na kuingia barabara kuu na nilipojaribu kumkwepa mzigo uliyumba na kusababisha gari langu kuanguka" alisema Mgeni.

Juhudi za mwandishi wa mtandao huu kusikia kauli ya dereva wa fusso ziligonga ukuta kwa kuwa hakuwepo eneo la tukio ingawa gari lake lilikuwepo.

                        PICHA NA Lost-9fm / GPL, MOROGORO

No comments: