May 8, 2011

MAISHA HAYA MPAKA LINI?????? MJENGONI MMETUSAHAU, HAYA NDIYO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?

Awamu ya kwanza ilipita tukawa tunajipa moyo kuwa awamu ya mr. ruksa itabadilisha maisha yetu lakini nayo pia ikapita, ikaja awamu ya utandawazi tukawa na fulsa ya kueleza matatizo yetu lakini awamu hii nayo pia haikusikiliza matatizo yetu. Kampeni ikafanyika hii ilikuwa ya mwaka 2005 na watu tulipigwa jua tukimsubiri mshindi kwa hamu. Haikuchukua muda mrefu kutangazwa kwa mshindi huyu akawa na sera ya maisha bora kwa kila mtanzania, miaka mitano hiyoooooooooo ikapita bila maisha bora tuliyokuwa tunayategemea. sasa miaka mingine mitano tukiwa tunaambiwa kuwa sasa ni kasi ya ajabu. Tunauliza hiyo kasi iko wapi?? ama kasi ya kutafuna mali ya umma???? Angalieni nani atatusaidia wagonjwa wetu wanapoteza maisha huku wakiyasubiria maisha bora kwa kila mtanzania. Lini yatafika kwetuuuu Kilulu Bariadi????????     By Lost-9fm

No comments: