Jan 6, 2011

MASTAA BONGO WAFANYIA UCHAFU CHINA!

Imedaiwa kwamba, baadhi ya mastaa wa Bongo, baada ya kukosa soko hapa nchini, wameamua kuamishia uchafu wao nchini China kwa kisingizio cha kwenda kufanya biashara, Amani linafumua.
Amani linathubutu kuanika uozo huo baada ya kujiridhisha na data kutoka kwa chanzo chake makini ambacho kinatonya kwamba wahusika wakuu ni mastaa wa kike wanaojifanya kuwa ni wafanyabiashara za nguo na vipodozi.

Ilidaiwa kwamba, katika listi ya mastaa wanaoongoza kwa shughuli hiyo, yuko mtangazaji maarufu wa kike (jina tunalo), mwanamuziki ‘the big name Bongo, na mastaa wawili wa kiwanda cha filamu huku aliyekuwa mshiriki wa kinyang’anyiro cha Balozi wa Kiswahili mwaka jana, Rehema Fabian ‘Video Queen’, akinyooshewa kidole.
Ilisemekana kwamba, Video Queen alitimkia nchini China kwa ajili ya kwenda kuchukua mzigo (bidhaa) yapata mwaka mmoja sasa hajarejea Bongo.

Ilielezwa kwamba, baada ya kufika nchini humo, miss huyo aliamua kuchukua makazi baada ya kufanya kilichompeleka ambapo ghafla bin vuu aliibukia katika mitandao mbalimbali ya watu maarufu akiwa na wazungu tofauti tofauti ndani ya Cassino maarufu za nchini humo.
Baada ya kuzitia kibindoni ‘nyiuzi’ hizo, lilimtafuta mnyange huyo ambaye alifafanua hali halisi nchini humo.

Katika maelezo yake, Video Queen yuko nchini humo kwa mambo binafsi ambapo alidai kwamba akiyakamilisha atatua Bongoland ‘suuni’.
Akifafanua juu ya skendo ya kunaswa na wanaume ‘daile’ na kuwekwa mtandaoni alisema: “Ni marafiki tu na si kama watu wanavyodhania, hata hivyo ‘kampani’ yangu kubwa ni ya wanaume.”

Video Queen alimalizia kwa kusema kwamba, suala la mastaa wa Bongo kwenda nchini humo kwa kisingizio cha biashara ni kweli lakini anawaasa kuachana na kukimbilia nchini humo wakidhani ndiko kwenye maisha ya kula ‘bata’ kwani yatawatokea puani.

No comments: