Mwanamuziki ‘front line’ wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ amenaswa akiwa ‘klozi’ na shemeji yake usiku wa manane, Risasi Jumamosi lina mikoba iliyosheni.
Staa huyo alibambwa na Paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Mzalendo Pub Millennium Towers, Kijitonyama, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii ambapo Bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa imeandaa sherehe maalum ya mastaa wa Bongo ‘Celebrity Party’.
CHALZ BABA AMPAKATA SHEMEJI YAKE
Stori nzima ilikuwa hivi; Mishale ya saa 12:30 usiku, Chalz Baba alipigwa chabo akiwa amempakata ‘sistaduu’ mmoja ambapo Risasi Jumamosi lilichezwa na ‘machale’ kisha kumfuata na kutaka kujua kulikoni.
CHALZ BABA AJIUMAUMA, AJITETEA
Katika kujiumauma, Chalz Baba alijitetea kwa kifupi huku akizima maswali zaidi: “Huyu ni shemeji yangu, ni ‘kifaa’ cha bosi wangu Omary Baraka.”
Baada ya majibu hayo, Chalz Baba alimzomea Paparazi wetu kwa kumwambia kuwa ‘imekula’ kwake kwani alidhani yule ni ‘demu’ wake hivyo ameambulia patupu.
Mwanzoni mwa mwaka jana, Chalz Baba alikuwa mwandani wa Wema Isaac Sepetu ambapo penzi lao liliiishia hewani baada ya mnyange huyo kutimkia nchini Marekani anakoishi na dada yake aitwaye Nuru Sepetu.
No comments:
Post a Comment