Sep 2, 2012

Wabunge wa AEC wazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuviomba  vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge hilo.Mbunge  wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Tasilimu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki  ambao wataufanyia kazi katika kikao cha  Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki  Abdullah Mwinyi akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa uwanja wa Ndege unaoendelea huko Taveta nchini Kenya kwamba hauna dhamira ya kuathiri uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Kulia ni Katibu  wa Wabunge hao  Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji .Katibu  wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Banji (kushoto) akiwaomba waandishi wa habari waweze kutangaza umuhimu wa Bunge hilo na fursa zilizopo kwa wajasiriamali hasa wanawake. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti Alhaj Adam Kimbisa  akifuatiwa na Angela Kiziga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira

No comments: