Sep 2, 2012

NORTH HOTEL KIWANJA BABKUBWA JIJINI MWANZA

Nimefika salama jana jijini Mwanza na kufikia katika kiwanja hiki kinachojulikana kama North Hotel ambacho kiko Kirumba Valey barabara ya Kitangiri ni kiwanja Bomba kina vyumba safi ambayo ni Self Contained na pia ni Full Air Conditioned na vinywaji mbalimbali vinapatikana hapo  jana, nimepata msosi babkuwa wa Samaki Sato na chipsi nilifurahia chakula hicho kwani nilikuwa nimemiss sana msosi huo , Mdau ukija mwanza hebu pitia hapo ujisikie duniani
Niko hapa kumuvuzisha matukio ya tamasha kubwa kabisa nchini la Serengeti Fiesta 2012 “Bhaaaaas” litalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza  na kushirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva.
Hapa nikiwa nimetulia katika ene la Mapokezi  nakuangalia  kitabu hiki ambacho kinaelezea migodi ya dhahabu ya Barrick huko Shinyanga.

No comments: