ELIZABETH MICHAEL ‘Lulu’
Ni staa mwenye umri mdogo ambaye alitikisa zaidi mwaka 2010. Aliandikwa kwa matukio yake ya kulewa kupita kiasi kwenye kumbi za starehe na kuvaa nusu uchi.
Lulu ambaye umri wake una utata, ikidaiwa yupo chini ya miaka 18, pia alihusishwa na matukio ya kimapenzi, kubwa zaidi likiwa lile la kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.
Kama hiyo haitoshi, aliripotiwa mwaka huu kugombana na ‘sidanganyiki’ mwenzake, wakidaiwa kurushiana makonde kisa kikiwa ni penzi la ‘janki flani’ hivi.

JACQUELINE WOLPER
Kati ya mastaa waliofanya vizuri kwenye soko la filamu Bongo mwaka 2010 ni Jacqueline Wolper lakini alitikisa kwa kuandikwa mara kwa mara akihusishwa na skandali mbalimbali.
Moja ya matukio hayo ni ile ya kudaiwa kutoka kimapenzi na chipukizi wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.
Tukio lingine ni lile alilodai kutaka kubakwa na mtu aliyemsema ni mjomba wake anayeitwa Exaud Macha.
Hata hivyo, baadaye Macha alidai kuwa Wolper ni mpenzi wake na hakuwa na lengo la kumbaka, isipokuwa msanii huyo alitaka kujimilikisha gari lake ndiyo maana alimdai.
Wolper alinaswa na skendo nyingine ambayo ilielezwa kwamba ‘alibondana’ na chipukizi wa filamu, Zuwena Mohammed Yusuf ‘Shilole’, ingawa baadaye walirekebisha tofauti zao.
REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’Staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ alinaswa na skendo kadhaa, moja ikiwa ile ya kudai kulazimishwa penzi na promota wa Kenya, Sadat Muhindi.
Hata hivyo, Sadat alikanusha skendo hiyo lakini Ray C hakurudi nyuma, kwani siku chache zilizofuata alitangaza kuachana na mchumba wake aliyedumu naye kwa zaidi ya miaka mitatu, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
Ray C a.k.a Kiuno Bila Mfupa pia mwaka huu aliandamwa na mzimu wa kuhama hama makazi kabla ya kuuza nyumba yake na kufungua duka, kisha ikaripotiwa kwamba amerudi nyumbani kwa mama yake, Bunju, Dar es Salaam.

AUNT EZEKIEL ‘GWANTWA’Super Character wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ aliandika historia mwaka huu kwa kuripotiwa kuhusika na skendo mbalimbali.
Moja ya matukio hayo ni lile la kugombana na msanii mwenzake wa filamu, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.
SYLVIA SHALLY
Miss Ilala 2009-2010, Sylvia Shally aliandikwa sana kupitia uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa filamu Bongo, Steven Kanumba.
MIRIAM JOLWA ‘KABULA’
Super-tall wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’, aliandikwa kwa skendo zake za kuvaa nguo ambazo zilimuacha wazi karibu asilimia 80 ya mwili wake.
Kabula ambaye aliitwa Jini kutokana na jinsi alivyomudu kucheza Igizo la Jumba la Dhahabu kwa nafasi ya jini, alivuma mwaka huu kwa uhusiano wake na Mfalme wa TAKEU, Nice Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ambaye baadaye waliachana kwa kukashifiana.

MR. NICE
Mbali na skendo ya Kabula, Mr. Nice aliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini baada ya kikundi cha watu fulani kumteka na kumpiga picha chafu ambazo walizisambaza.
KHALEED MOHAMED ‘TID’
Mkurugenzi wa Top Band, Khaleed Mohamed Salum ‘TID’ kwa mara nyingine, mwaka huu aliingia kwenye ‘kashkash’ za kupigana, mojawapo akiripotiwa kumtwanga mrembo mmoja jijini Dar.
HASHEEM THABEETThe 7.3 ft, Hasheem Thabeet Manka, alivuma na skendo yake moja ya ‘kumzibua’ TID mpaka staa huyo wa Bongo Fleva akazimia.
Hasheem anayevaa jezi namba 34 akiwa na Klabu ya Basketball ya Memphis Grizzlies inayocheza Ligi ya NBA, Marekani alipoulizwa kuhusu kumpiga TID alisema kuwa staa huyo wa Zeze alimchokoza.

BONIFACE AMBANI
Aliwika akiwa na Klabu ya Yanga kwa misimu miwili mfululizo, 2008-09 na 2009-2010 kabla ya kuondoka, akiwa nchini alivuma kwa uhusiano wake wa kimapenzi na msanii wa filamu nchini, Flora Mvungi.
NELLY KAMWELUNi Miss Ilala namba 2 2008-09, pia alifanikiwa kutinga 10 Bora ya Miss Tanzania mwaka huo, skendo zake mwaka huu zilikuwa nyingi, akiripotiwa kuchapa kilevi ‘kwa sana’ mpaka kupoteza ‘network’.
NASEEB ABDUL ‘DIAMOND’Mwaka huu alitoka vema kimuziki lakini baada ya kulamba tuzo tatu za KTMA Mei 14, 2010 pamoja na ‘dili’ la ubalozi wa malaria, alianza kuchangamkia skendo akianza na kutoka kimapenzi na Wolper.
Diamond pia alihusishwa na ‘kashkash’ za mapenzi na warembo, Rehema Fabian ‘Balozi wa Kiswahili’, mshiriki wa Miss Tanzania, Amisuu Maliki na Upendo Mushi aliyeshiriki Maisha Plus.

JOSEPH SHAMBA ‘VENGU’
Hivi sasa amesimamishwa kwenye kundi lake la Orijino Komedi na sababu ya kupigwa ‘suspensheni’ ni skendo mfululizo lakini zote zikiambatana na ulevi wa kupitiliza.

No comments:
Post a Comment