Tatizo, pengine ni hisia kwamba waanzishaji haya matawi ya chama nchi za nje, hasa ya CCM, ni wasaliti wa watanzania wengi ambao ni masikini. Hilo linatokana na matarajio kwamba Mtanzania ambaye amefanikiwa kutoka nje ya nchi amepanuka kimtazamo na kwamba mtu ambaye amepanuka kimtazamo na ana ujasiri, hawezi kukiunga mkono CCM, chama ambao kimekuwa madarakani muda mrefu bila kuleta maendeleo ya kweli kwa mtanzania masikini.
Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Michael Ndejembi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Houston, Texas ili kufahamu mtazamo wake juu ya uanzishaji wa matawi ya CCM nchi za nje.
Jiunge nasi kwa kupitia hapa: http://www.radiombao.com
Click here to listen live: http://cp.radiostreamhost.com/
Ahsante,
Utawala,
http://www.radiombao.com
No comments:
Post a Comment