Jan 6, 2011

Eliza agoma kuizungumzia ndoa yake

STAR wa Big Brother Africa 2009, Elizabeth Gupta juzikati aligoma kuzungumzia masuala ya ndoa yake na mchumba wake Kevin Chuwang Pam, inayotarajiwa kufungwa siku za hivi karibuni.

Ishu hiyo ilijitokeza usiku wa kuamkia Desemba 29, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya nne ya mwanamuziki Khaleed Mohamed ‘TID’ baada ya kufuatwa na Paparazi wetu aliyetaka kujua lini wawili hao watachukuana jumla.

Paparazi wetu akipiga stori na Eliza, alihoji lini wanatarajia kufunga pingu za maisha lakini mwanadada huyo alikataa katakata kuzungumzia suala hilo akidai kuwa, wakati wa kufanya hivyo bado.

“Suala la ndoa kwa hapa siwezi kulizungumzia ila muda ukifika nafikiri mtafahamu maana kila kitu kitakuwa wazi na hakutakuwa na kificho chochote so utanisamehe kwa hilo,” alisema Eliza.

Wakiwa ukumbini hapo Eliza na mchumba wake huyo, muda mwingi walionekana wenye furaha kwani mara kwa mara Kevin alipanda stejini na ‘kuchana’  mistari sambamba na TID.

Kwa upande wa Eliza, naye hakumuangusha mchumba wake kwa kwenda kumtuza kufuatia umahiri wake wa kuimba jukwaani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilicho karibu na familia ya akina Eliza, vikao vya sherehe ya kumuaga binti huyo ‘send off’ itakayofanyika Januari 2, mwakani jijini Dar es Salaam vinaendelea na kufuatiwa na ndoa itakayofungwa nchini Nigeria anakotoka Kevin.

Baadhi ya ndugu wa Kevin tayari wapo nchini kuhudhuria sherehe hiyo.

No comments: