Jan 6, 2011

Dude: Nimechoka na skendo bora nioe

Staa wa kipindi cha Bongo Dar es Salaam kilichokuwa kikirushwa katika Runinga ya TBC1, Kulwa Kikumba ‘Dude’  (pichani) amesema kwamba Mei 2011 atafunga ndoa ili kuepukana na skendo ambazo zimekuwa zikimuandama.

Dude alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori na paparazi wetu katika Ukumbi wa Mango Garden uliopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Akifafanua juu ya uamuzi wake huo, msanii huyo alisema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na mwaka 2010 kuandamwa na skendo kadhaa.

“Nimechoshwa na skendo zilizonikumbuka mwaka huu, kudhidhibiti zisitokee tena nimeamua Mei mwakani kufunga ndoa na mchumba wangu Eva,” alisema Dude.

Aidha, Dude aliongeza kuwa, kama Mwenyezi Mungu atamjaalia mipango yake kwenda vizuri, anatarajia kufunga ndoa ya kihistoria katika maisha yake.

Magazeti ndugu na hili Amani na Risasi Jumamosi, yaliwahi kuripoti habari za staa huyo ambapo Amani la Desemba 16, 2010 liliripoti kuwa sherehe ya Mike, Thea, Dude, mkewe nusura wazitwange ukumbini na Risasi Jumamosi la Desemba 18, 2010 liliripoti habari iliyokuwa na kichwa kisemacho ‘Kumbe Adui wa mume wa Uwoya ni Dude’.

No comments: