Jun 14, 2013

"WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..NATAMANI KUACHA MUZIKI ILI NIYANUSURU MAISHA YANGU"....SHILOLE

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha kufikiria kuachana na kazi hiyo.

Akiongea na mwandishi wetu pasipo kuwataja  wabaya  wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’ za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.

“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,”
alisema Shilole.

No comments: