Jun 20, 2013

"TUKIO LA ARUSHA LIMENIFANYA NIAMINI KUWA TANZANIA KUNA WANARIADHA WAZURI".....HUU NI UTUMBO WA MBUNGE SERUKAMBA


Tukio la bomu la Arusha  limewasitua wengi  kufuatia  vifo  vya  wananchi  wanne  wasio  na  hatia....

Nasema  hawana  hatia  kwa  sababu  siku ya  tukio  wananchi  hao  walikuwa  katika  mkutano  wa hadhara wa  chama  chao  ( CHADEMA )  sawa na ambavyo  wangeweza  kuwa  katika  mkutano  mwingine  wowote  wa  kisiasa....

Pamoja  na  majonzi  waliyonayo  wananchi, wanasiasa wetu  wanaonekana  kutoguswa  kabisa  na  vifo  hivyo  ambavyo  kwa  mtazamo  wangu  nathubutu  kusema  kuwa  chanzo  cha  yote  ni  wao .....

 Jana kupitia  account  yake  ya  twitter, mbunge  Serukamba  alidai  kuwa  tukio   la  Arusha  halimpi  fundisho  lolote  zaidi  ya  fundisho  moja  tu  kwamba  TANZANIA  KUNA  WANARIADHA  WAZURI.....

Tunapata  fundisho  gani  hapa???... Ndugu zetu  wamekuwa  wakipoteza  maisha  kila  mara  kupitia  mikutano  ya  wanasiasa wetu....

Cha  kushangaza  ni  kwamba, wanasiasa  haohao wamekuwa  wakitucheka  na  kutudhihaki...!!!

Kauli hii  ni  fundisho  tosha.
 

Najaribu  kuihusisha  kauli  ya  mbuge  huyu  na  tusi  la  nguoni  alilowahi  kulitoa  bungeni  la  "COME ON  FU**K  U"...ili  nimjue  alivyo

Matukio haya  yanatosha  kumpima  Serukamba  na  kumjua  jinsi  alivyo...!!!

No comments: