Jun 15, 2013

PICHA ZA SHOW YA LADY JAYDEE NYUMBANI LOUNGE.... WATU WALIJAA MPAKA WAKAANZA KUBEBANA

Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki. 
DSC_4275

Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya, Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni picha za show hiyo.

Umati wa watu unaoshuhudia show ya Lady J Dee sasa hivi hapa Nyumbani Longe.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Professa Jay akiwa back stage anajiandaa kupanda jukwaani kutoa burudani nzuri kwa mashabiki
 

Miaka 13 ya Lady j Dee#sasa hivi ndiyo Mh.Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ameingia

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Team Times Fm 100.5 (Dj Jors Bless,Ndimbo na Mariam)

Sugu na Mkoloni wanatoa burudani kali kwa mashabiki.

Mama mzazi wa Lady J Dee naye amekuja kushuhudia show ya mwanae.

Juma Nature anatoa burudani kwa mashabiki

Sugu akitoa burudani kali kwa mashabiki
M 2 The P akiongea machache baada ya kukaribishwa kwenye jukwaa na Juma Nature.
 
Hivi ndivyo hali ilivyo ndani ya Ukumbi huu wa Nyumbani Lounge,Namanga jijini Dar es Salaam ambapo leo hii kuna bonge moja la show la Mwanadada mkongwe kwenye tasnia ya muziki hapa nchini,Lady Jay Dee ambaye anatimiza miaka 13 tangu alipoanza kazi yake ya muziki.katika show hii wanamuziki mbali mbali wamepanda jukwaani akiwepo Mh. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.

 Wadau mbali mbali wa muziki hapa nchini wapo ndani ya ukumbi huu kusuhudia show hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki.
 Ndani ni nyomi la hatari,lakini nje nako watu bado wanataka kuingia huku wengi wao wakisema kuwa "hata kama hakuna siti,sie tuko radhi kusimama ilimradi tumsapoti Dada yetu."
 Getini mambo yako namna hii.
 Foleni bado ni ndefu na watu bado wanazidi kuingia ukumbini hapa hivi sasa.
Burudani ya Utangulizi ikiendelea.

No comments: