Aliyekuwa mshindi katika shindano la kumtafuta mrembo wa wilaya ya
Nyamagana jijini Mwanza, Redd’s Miss Nyamagana 2013 Diana Amimo
amevuliwa taji hilo baada ya kubainika kudanganya umri wake pamoja na
urai, kasoro zilizompunguzia sifa za kuvaa taji hilo.
Mratibu wa shindano hilo lililofanyika (May 11) jijini Mwanza, bwana
Mukhsin Mambo wa Stoppers Entertainment, ameeleza kuwa baada ya
kugundua mapungufu hayo kwa Diana, kamati ilikaa (June 6) na kuamua taji
hilo kumvisha aliyekuwa mshindi wa pili Rosemary Peter ambaye sasa
ndio Redd’s Miss Nyamagana 2013.
Rosemary Peter (Reds Miss Nyamagana 2013 wa sasa)
Mr. Mambo amesema udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na
idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza wiki moja baada ya shindano hilo, baada
ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo na kubaini kuwa
Diana ni raia wa Kenya na ana umri wa miaka 17.
Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24
No comments:
Post a Comment