Jun 13, 2013

MSANII MATONYA AFIKISHWA MAHAKAMANI HUKO SONGEA KWA TUHUMA ZA UTAPELI....HUU NDO MKASA WAKE


Msanii Matonya  amekamatwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliopo manispaa ya Songea mkoani ruvuma. 

Taarifa  zinadai  kuwa  Matonya  aliingia ukumbini akiwa amelewa,  hali iliyomfanya  ashindwe  kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi  huo baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo...


Baada  ua  hali  hiyo,  waandaaji wa show hiyo waliamua  show  hiyo  ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia .

Mbali na sakata hilo, Matonya alitakiwa akafanye show nyingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivyo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam ....

 Baada ya kuvuja taarifa hizo , waandaji walimfuata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu nyingine. ...

Walipomkosa, waliamua  kumvizia katika  stendi  ya mabasi ambako  walifanikiwa  kumkamata  akijiandaa  kusepa..!!!


Hadi sasa, msanii huyo  yupo mahakama ya mwanzo ...

No comments: