Jun 25, 2013

HILI NDO JENERATA LINALOTUMIA MKOJO BADALA YA MAFUTA....LILIGUNDULIWA MWAKA JANA NA MABINTI WANNE

WASICHANA wanne kutoka Nigeria wamegundua jinsi ambayo mkojo unaweza kutumika kama mafuta ya kusukuma jenereta. 
 
Wasichana hao, Duro-Aina Adebola,Akindele Abiola, Faleke Oluwatoyin na Bello Eniola, wote wenye umri wa miaka 14 walifanya maonyesho ya jenereta hilo na lilionekana kufanya kazi  mwishoni  mwa  mwaka  jana


Genereta hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k..
 
Genereta hilo linafanyaje kazi?

Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo kiitwacho electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen. Kisha hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji kwaajili ya kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.

Hiyo gas cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa, liquid borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi.

No comments: