SHINDANO la Big Brother Afrika limeendelea kwa washiriki wawili kutolewa katika wiki ya kwanza ya mchezo huo ambao unashirikisha washiriki wapatao 28 kutoka nchi 14 barani Afrika.
Jumatatu iliyopita washiriki walipata nafasi ya kutoa mapendekezo yao ya kuchagua washiriki ambao wanaona wanafaa kuingia katika Danger Zone ambapo watano kati yao ndio waliotajwa mara nyingi zaidi na washiriki wenzao hivyo kuingia huko.
Washiriki waliongia katika Danger Zone walikuwa ni Betty wa Ethiopia, Selly wa Ghana, Denzel wa Uganda, Natasha wa Malawi na Huddah wa Kenya ambapowatazamaji walitakiwa kumpigia kura mshiriki ambaye wanaona anafaa kubakia ndani ya jumba hilo.
Katika
kura zilizopigwa na watazamani kutoka nchi 14, Betty ndio alipata kura
nyingi zaidi baada ya kupata kura 5, akifuatiwa na Selly na Natasha
waliopata kura tatu kila mmoja huku Denzel na Huddah wao wakiambulia
kura mbili hivyo kumaanisha kwamba safari yao katika kugombea dola
300,000 kuishia hapo.
Baada
ya kutolewa katika jumba hilo IK mtangazaji wa kipindi hicho aliwapa
nafasi washiriki hao kulipa kisasi kwa kuchagua mshiriki mmoja ambaye
hupewa kazi ambayo hutakiwa kuifanya kwa muda atakaopangiwa.
Wa
kwanza alikuwa Denzel ambaye alitakiwa kuchagua mshiriki ambaye
atatakiwa kila akitoka nje kupunga hewa kwenye jumba hilo awe anatembea
kwa miguu na mikono kwa muda wa siku tano na kijana huyo hakusita
kumchagua Nando mshiriki wa Tanzania kufanya kazi hiyo.
Aliyefuata
alikuwa na Huddah ambaye yeye aliambia achague mshiriki ambaye atakuwa
akitandika vitanda vyote katika jumba hilo kwa muda wa siku mbili na
mwanadada huyo mrembo kutoka Kenya alimtaja mwanadada mwenzake Dillish
kutoka Namibia kufanya zoezi hilo.
Shindani
hilo linaendela tena leo ambapo washiriki watatakiwa tena kupendekeza
majina ya washiriki ambao wataingia katika Danger Zone kwa ajili ya
kupigiwa na mashabiki ambapo atakayepata kura chache ataliacha Jumba
hilo Jumapili ijayo.
pro24
No comments:
Post a Comment