May 5, 2013

PICHA ZA JENGO LINALOFANANA NA UUME ZATOLEWA NA GAZETI LA CHAMA TAWALA NCHINI CHINA...


Gazeti la chama tawala cha china, People’s Daily ambalo limezoea kuwa kitovu cha kusambasa habari, sasa limejikuta likiwa habari baada ya watu wenye fikra za kitukutu kuona jengo jipya la gazeti hilo limefanana na nyeti za kiume.
 
Jengo hilo lenye urefu wa mita 150, hivi sasa bado linaendelea kujengwa jijini Beijing. Kutokana na muundo huo usiokua wa kawaida, picha za kibunifu zikaanza kuibuka katika website ambayo ni kama “Twitter ya China,” inayoitwa Sina Weibo.
Watu wengi wameeleza kuwa kwa kutumia ubunifu kidogo tu wa photoshopping, unaweza kuambatanisha picha ya jengo hilo, ambalo raia wamelipa nickname “Giant Pen*s” au “Uume mkubwa,” katikati ya “miguu” ya jengo lingine maarufu nchini humo ambalo ni makao makuu ya kituo cha TV cha China Central Television (CCTV,) linalojulikana kwa nickname ya “Big Und*rpants” building au Jengo la Chupi Kubwa.
 Habari za utani huo zilifikia wakubwa nchini humo ambao walikerwa na kuamua kuwaharibia watu raha zao kwa kuamuru website ya Sino Weibo ku-block search zote zinazotafuta picha au habari za jengo hilo. 
Kwa sasa Wachina wakitafuta jengo hilo, wanakutana na ujumbe “kuendana na sheria, kanuni na sera husika, matokeo ya utafutaji wako (search results) hayawezi kuonyeshwa."
 
Mwandishi wa Reuters, Anita Li amesema “hii inaonyesha frustrations miongoni mwa vijana watumiaji wa internet nchini China, na pia inaonyesha ni kiasi gani “wakubwa” wako sensitive kwa hata vitu vidogo vya kipuuzi online.”
source: mpkekuzi blog

No comments: