Walio wengi wamezoea
kusikia ufisidi katika siasi, viongozi waliokua na
uuzo wa tabia na
kujilimbikizia mali chungu nzima. Ufisadi hauishii
kwenye siasa tu bali kuna
ufisadi kila sehemu, kwenye kazi, mashirika
binafsi, michezo na hata
katika tasnia ya muziki. Ufisidi katika tasnia ya
muziki upo, tena mkumbwa
na si rahisi kuusikia wala kuuona hata
ukiwa msaani.
Swala hili la ufisadi
katika muziki tumekuwa tukilifatilia kwa muda sasa
kama wadau wamuziki na
tumefanya uchanguzi wa kina sana kwa
kuongea na watu tafauti
tafauti katika mziki, wasanii, maproducer, ma
presenters, ma dj na wadau
wa mziki.
Tumekua tukisikia
malalamiko mengi sana ya wasanii hivi karibuni
kwanini nyimbo hazipingwi?
Kwanini hawapati show? Na maudhi
mengine mengi. Hivi sababu
nini hasa ? Nyimbo zao ni mbaya?
Hawana vipaji au? wasanii
kama chidi benz, lady jd, ali kiba, bushoke,
prof jay, matonya,
makamua, qchief, TID, na wengine wengi. Kuna
jambo hapa japo kua wengi
hawataki kulizungumzia kwa kuogopa au
labda kwa ufahamu mdogo.
Nyuma ya yote haya kuna mafisadi,
hawa ni watu ambao
wanaupeleka mziki wanavyotaka wao kwa
kujifanya kama wao ndio
wamiliki wa huo mziki na kutumia nafasi zao
za kazi vibaya kwa manufaa
yao binafisi bila kujali mustakabali wa
tasnia ya muziki.
Kuna kijikampuni kinaitwa
OSATA ambacho kazi yake kubwa ni
promotion, publishing na
usimamizi wa wasanii tafauti tafauti kwa njia
ya mikataba mifupi mifupi.
Wamiliki wa kampuni hiyo ni Babu Tale, Said
Fela na Suka Othumani Suka, OSATA ni ufupisho wa majina haya
matatu.
Herufi O katika OSATA ni
Othuman suka ambaye ni mfanyakazi wa
cloudfm kwenye upande wa
kusikiliza /kuhakiki nyimbo za wasanii na
kuzipitisha kabla ya
kupigwa.
Na herufi SA katika OSATA ni
said fela ambaya ni meneja wa kundi la
Tmk Wanaume family ,
Herufi za mwisho TA katika
OSATA ni Tale ambaye pia ni manage wa
kundi la Tip Top
connection.
Kazi kubwa ya kampuni hii
ni kusambaza muziki kwenye redio,
television, mitandao ya
jamii na sehemu nyingine nyingi. Kampuni hiyo
haiishi kwenye kusambaza
tu bali inafanya promotion ya hizo kazi
walizosambaza kwa kutumia
pesa au lugha nyingine fasaha rushwa.
Rushwa kwa maana kuwapa
mapresenter na madj wa redio tafauti
tafauti pesa kupiga hizi
nyimbo wanazozipromote. Katika uchunguzi
wetu kampuni hiyo inamtoza
msanii kiasi cha shilling mil 3 kusambaza
na kufanya promotion ya
nyimbo. Kwa haraka haraka unaweza
kusema hakuna tatizo,
OSATA inafanya biashara tu na hakuna ofisadi
wowote ule unaendelea.
Katika shughuli hizi za promotion ya nyimbo
katika redio na
television, OSATA huwalipa madj na wafanyakazi wa
media kupiga kazi zao na
pia kuwashawishi kutokupiga kazi za watu
wengine ili wapate wateja
wengi katika kampuni yao.
OSATA inamtandao wa
wanahabari nchi nzima, wafanya kazi hawa
wa redio na television
hulipwa ilikupiga video na nyimbo zaidi ya
kawaida. Tatizo linakuja
pale ambapo nyimbo mbaya inapewa nafasi
na nyimbo bora haipigwi
kabisa kwasababu OSATA imelipia promotion
kabambe. Kibaya zaidi ni
pale mfanyakazi wa redio anapokua ni
mmoja wa miliki wa kampuni
ya usambazaji ambae ni Suka Othumani
suka, unafikiri kutakua na
haki kweli kwenye upangiliji wa nyimbo
kwenye ratiba ya redio?
Unafikiri nyimbo yako itapita kweli kama
hujalipa kwa OSATA ili
ufanyiwe promotion? Sanaa inakuwa vipi kwa
hali hii? Lazima msanii
alalamike kwa hali hii kwababu huwezi kupata
show bila muziki wako
kusikika. Huwezi kuendesha maisha kama hupati
angalau show moja katika
mwezi, unaposikia msanii kaingia katika
madawa ya kulevya
msimcheke tu bali kuna mambo mengi katika
muziki yanachangia
kumpoteza msanii na hili ni moja wapo.
Operesheni za OSATA
zinaendeshwe kisiri siri sana na wamiliki
wanaotambulika ni babu
tale na saidi fella, huku wakimtaje othumani
wakijuafika jina hilo
halitambuliki kwenye umma.
Angalia interview hii
kwenye youtube ya kipindi
cha sporah babu tale akimtaja othumani
na saidi fella
http://www.youtube.com/watch?v=uTgt_lRNQBE
dakika 17 sekunde
40. Katika interview hiyo
babu tale anaizungumzia OSATA jinsi
invyofanya kazi na
redio/TV.
Jina hili la othumani
limetumika ili isijulikane kuwa huyo mtu ni suka
othumani suka ambaye ni
huyu hapa katika facebook account
Osata inatumia nyundombinu
za clouds FM na Television kufanya
promotion hizo za mziki
kupitia mgongo wa suka . Mikutano ya OSATA
hufanyika THT (Tanzania
House of Talent) na office za cloudfm, ukifatilia
kwa karibu unaweza
ukadhani OSATA ni operesheni ya redio hiyo,
mameneja hao hujichanganya
kama wafanyakazi ukiwaona unaweza
usiwatafautishe na wafanya
kazi cloudsfm.
Sisi kama wadau wa muziki
baada ya kufanya uchunguzi wa kina
tunaamini kabisa hii ni
kazi ya ruge mutahaba baada ya kuona
Tanzania fleva Unit
imefeli na kujiondoa katika picha mbaya katika
tasnia ya muziki. Osata
nikama chombo ambacho kinatumika tu na
THT/Ruge Mutahaba
kucontrol muziki na media nyingine kwa ajili ya
manufaa yake binafsi. Kila
show utakayoenda lazima umkute, mwasiti,
linah, barnaba, chege,
made, tundaman, n.k – haimanishi kua hawa ni
wasanii bora Tanzania bali
ndio wanaosambaziwa kazi zao na hili kundi
la mafisadi. Akitokea mtu
mwingine anayejifanya anasambaza na
kufanya promotion anazimwa
haraka sana kwa fitna na mipango ya
osata.
Osata imefika mpaka
mmalaka ya kuwaambia ma presenter
wasipinge nyimbo ya baadhi
ya wasaanii hapa nchini kwa lengo la
kuwapoteza ili waende
kulipia promo. Kila mtu analia kivyake ila
hamna mtu anayetaka
kuongelea ukweli kwa kuuogopa ,Osata, ruge,
THT and Cloudfm. Hii media
house ilipata stress kubwa sana kipindi cha
Bwana Sugu na Anti-virus,
kulikua hamna amani mjengoni hata
mahudhurio ya matamasha
hayakua mazuri. Kwa kutumia njia zake za
kifisadi ruge mutahaba
akaweza kuuzima moto- akaihusisha serikali
kwa kumpeleka sugu bungeni
ili wapate suluhisho, kumbumbukeni
mnachezea maisha ya watu,
mnaharibu kazi za watu, kujifanya nyie
ndio wamiliki wa muziki
mtakuja kuumbuka vibaya sana mbele ya haki.
Hii tahadhari kwa vituo
vya redio, television, magezeti na vyombo vya
habari vyote kuwa kuna
ofisadi unaendelea, hili hundi na washiriki
wake wanatumia pesa
kuendesha vyombo vyenu. Fanya uchunguzi
wako binafsi utaona
mwenyewe, kabla ya matamasha makubwa
utaona video na nyimbo
flani za wasanii flani zinapigwa kweli na ndio
hao hao utawakuta kwenye
matamasha. Osata, ruge, cloudsfm na tht
nia yao ni kuucontrol
muziki. Sisi kama wadau wa muziki tunasema
haiwekani kabisa.
Huu ni ufunio wa kwanza tu
tunaendelea na uchunguzi, kuna nyaraka
nyingi zinakuja na
tutaziwakilisha kwa jamii zikiwe zimeambatana na
interviews. Joseph Kusaga
moto unaanza tena huu usije ukatoa
lawama tena, hakuna
atakayekusikiliza mara hii sababu unawaachia
vijana wanafanya ufisadi
kwenye ufalme wako. Kama ulikua hujui basi
natumia umeujua ukweli.
No comments:
Post a Comment