BARAZA LA VIJANA CHADEMA JIMBO LA KAHAMA LANENA KUHUSU HUJUMA YA UCHAGUZI WA MABARAZA YA KATIBA KAHAMA..
MWENYEKITI WA BAVICHA KAHAMA SHIJA BENEDICT
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA
JIMBO LA KAHAMA, S.L.P 922 KAHAMA
BARAZA LA VIJANA JIMBO LA KAHAMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
HUJUMA NA UKIUKWAJI MKUBWA WA TARATIBU ZA KUWAPATA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA/HALMASHAURI YA MJI-KAHAMA
CHADEMA jimbo la Kahama,Kupitia Barazala la Vijana Chadema-BAVICHA Kahama,
inapenda kuufahamisha umma wa Kahama na
Watanzania wote kuwa; Tumesikitishwa sana na hujuma zilizofanywa na CCM wilaya
ya Kahama chini ya uratibu wa katibu wao wa wilaya Bw. Michael Charles katika mchakato mzima wa upatikanaji wa
mabaraza ya katiba ya wilaya.
Ndugu Wanahabari na
Watanzania wenzangu,
Kwanza, Miongoni mwa hujuma hizo ni pamoja na kuwatisha watendaji na kuwashurutisha kufuata maelekezo ya CCM,Yaliyohusu
wagombea wanaotakiwa na CCM na si
wanaotakiwa na Wananchi,katika mpango huo CCM iliwaita vitongoji wote,
wenyekiti wa mitaa kuwapa majina manne yaliyopitishwa na kamati za siasa za kata za CCM katika
wilaya ya Kahama.
Pili, katika maeneo ambayo
Hakuna Vitongoji wakuchaguliwa au Wenyeviti wa mitaa, CCM ili kuainisha nafasi
hizo kwa watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi kinyume na Sheria ,Hata pale Wananchi
na Wagombea walipo hoji watendaji wa
kata waliwapuuza kwa hofu ya vitisho toka CCM.
Tatu ,katika maeneo ambayo Mpango wa CCM ulipuuzwa na Vitongoji au Wenyeviti wa
mitaa ,ilihali idadi kubwa ya Vitongoji,Wenyeviti wa mitaa wakitokana na
CCM,CCM iliwaamuru watendaji kupeleka karatasi za kura katika ofisi ya CCM
Wilaya ili kutambua ni akinani walio saliti mpango huo,Eti kwa kile kinachoitwa hatua za kinidhamu za kichama,Watanzania,kitendo
cha kutambua kura hizo ni uhalifu,umafia na hujuma kwani kura hizo zilikuwa za
siri na kwa vyovyote vile ni kinyume cha sheria na Taratibu za Tume ya Maoni ya
Katiba,kutoa siri za kura,pia ni uchochezi na hatari kwa usalama wa wahusika.
Nne ,Ni wazi kuwa Wenyeviti wa mitaa/vitongoji walikuwa na wajibu wa kupigia kura Wananchi, baada
ya kuwahoji na kupima uwezo wao wa
kujadiliana kupambanua mambo kupitia maelezo na wasifu wa
Wagombea/Waombaji, kitendo kilichofanywa na vitongoji katika kata ya Nyihogo
kwa wao kama Wenyeviti kugombea nafasi za ujumbe huku wakiwa na (interest) katika W.D.C hakikubaliki na
ni unyimaji wa haki kwa wananchi wasio na “interest”na
Baraza la maendeleo la kata (W.D.C), moja kwa moja.Pia kitendo cha
kupitisha majina ya watu ambao hawa kuhojiwa wala kutoa maelezo, ilikupima uwezo wao ni uvunjaji wa taratibu,nani
hujuma,CCM katika hili imefanya na inafanya umafia, kinacho shangaza nikuachwa
kwa kundi kubwa la Wasomi na Wataalamu
wa Fani mbalimbali ikiwemo,wasomi wa sheria,badala yake na kwa-misingi ya Kisiasa,
Umafia na Uhuni wa CCM Wajumbe takribani asilimia 80% ni Darasa la saba na hawajui
chochote kuhusu Katiba,ila kungoja maelekezo toka CCM,,Huu ni Umafia na Uhuni
wa makusudi dhidi ya Watanzania,hasa Wanakahama.
Tano, kitendo cha mtendaji wa kata ya Mhongolo
kutoshughulikia malalamiko ya wagombea kabla ya zoezi la kuwahoji kuanza,juu ya
uhalali wa kitongoji cha NYAMHELA kuwakilishwa na mtu ambaye hakuchaguliwa na wananchi Bw.Amos Jikala kwa maelekezo ya CCM, Huku
ni kunyima Haki, Uchochezi na matumizi mabaya ya ofisi ya umma kwa mujibu wa
sheria za Nchi. BAVICHA kwa niaba ya CHADEMA
Jimbo la Kahama tunaomba wananchi
watuunge mkono katika hatua zote zitakazo chukuliwa na CHADEMA Taifa juu ya
Umafia na Hujuma ya CCM kwa Watanzania.
Sita, Kitendo cha kihuni kilichofanywa
na mtendaji wa kata ya MHONGOLO Bw. Emmanuel
Kalolo ,kuchakachua maamuzi ya W.D.C (Baraza
la Maendeleo la Kata),kwa kubadili muhtasari tena ndani ya ofisi ya CCM Wilaya ya Kahama na kuwasilisha majina katika ofisi ya
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji,majina yaliyoelekezwa na CCM,Yasiyo tambuliwa na W.D.C na ambayo Diwani kama mwenyekiti wa W.D.C hakusaini,kitendo cha kubandika
majina ya washindi katika mbao za matangazo
na kisha kuandika muhtasari wenye majina mengine ni Umafia,Uchochezi,
Unyimi wa Haki na matumizi mabaya ya ofisi za Umma.
Saba, kitendo chakaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji Bw. Felix Kimario,
kutumiwa na CCM kufaniksha Umafia wao,Ni kinyume na sheria, Watanzania !!!
Baada ya watendaji waadilifu kwa Umma kukataa maelekezo ya CCM katika mkakati
wao wa kimafia wa kuhujumu Maoni na maamuzi ya Wananchi , CCM walitumia ofisi ya
kaimu Mkurugenzi ,kwa kutuma baadhi ya maafisa wa Umma kutekeleza mpango wa
kihatifu wa CCM.Hata baada ya watendaji hao waadilifu kushikilia misimamo na
miiko yao ya kazi ,kaimu Mkurungenzi huyu wa Halimashauri ya Mji wa Kahama
,aliamua kuangiza Watendaji hao waadilifu kutoa nyakara mbalimbali zinazohusu
zoezi hilo ikiwemo kura za siri.Eti kwa utambuzi katika ofisi za CCM Wilaya
,Huu ni Uhuni,Umaifa ,Unyimi wa Haki na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma.
Hitimisho, Baraza
la vijana Jimbo la Kahama kwa niaba ya Chadema Jimbo la Kahama tuna laani
vitendo hivyo vya kihuni,Kimafia ,Unyimi wa Haki na Matumizi mabaya ya Madaraka
na Ofisi za Umma.Ninachukua wasaha huu
kuwaomba wana kahama na Umma wa
Watanzania kutuunga mkono katika kila hatua, Itakayochukuliwa na Chadema Taifa
kwa maslahi ya Taifa, Ya leo na ya kizazi
kijacho.
No comments:
Post a Comment