Mar 12, 2013

FILAMU YA KINA BABY MADAHA, CHILLO YAPATA TUZO


Mzee Chillo akiwa ameshikilia tuzo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Baadhi ya wasanii walioshiriki katika filamu hiyo, Mama Mjata (kushoto), Baby Madaha (katikati) na Mzee Chillo (kulia).…
Mzee Chillo akiwa ameshikilia tuzo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).
Baadhi ya wasanii walioshiriki katika filamu hiyo, Mama Mjata (kushoto), Baby Madaha (katikati) na Mzee Chillo (kulia).
Wasanii na wafanyakazi wa Pilipili Entertainment wakifurahia tuzo hiyo.
                                                       Baby Madaha akiwa ameshikilia tuzo.
FILAMU iliyotawaliwa na wakongwe kibao katika fani ya uigizaji Bongo ya ‘Ray of Hope’ imepata tuzo ya baada ya kushindanishwa na filamu kibao za hapa nchini na nje ya nchi katika shindano lililokuwa linaendeshwa na Africa Magic.
Filamu hiyo ambayo ni mali ya kampuni ya Pilipili Entertainment imechezwa  na wasanii wakongwe kibao akiwemo Mzee Chillo, Hashimu Kambi, Mama Mjata, Pastor Myamba, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Baby Madaha na Kennedy ‘Kenny’.
Akizungumza mbele ya mapaparazi katika ofisi za kampuni ya Pilipili Entertainment, Mzee Chillo alisema hii ni mara ya pili filamu hiyo kuchukua tuzo kwani ya kwanza ilikuwa ni ya ZIFF mwaka juzi.                                          

No comments: