Aug 19, 2012

TAARIFA KAMILI KUHUSU MGANGA ALIEKAMATWA NA MABOMU TABORA.

.
Mtu mmoja aitwae Msindi Kasaki anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 68 mkazi wa kata ya Ololangulu wilayani Uyui mkoani Tabora, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na mabomu manne nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Anthony Rutta amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo anaesadikiwa kuwa ni mganga wa tiba za asili kumefanikiwa baada ya taarifa kutoka kwa msamaria mwema.
Amesema baada ya hizo taarifa askari walikwenda kwenye eneo hilo ambapo baada ya upekuzi na kumuhoji, Msindi alikiri kuhifadhi mabomu hayo ambayo alikua ameyachimbia chini ya ardhi nyuma ya nyumba yake yakiwa ni mabomu manne ya kutupa kwa mkopo ndani ya mfuko.
Kamanda Rutta ameongeza kwamba utafiti uliofanywa na polisi inasemekana hayo mabomu yaliagizwa nchi jirani na lilikua limeandaliwa tukio kwenda kufanya uhalifu kwenye mnada mmoja mkoani Tabora.

No comments: