Aug 19, 2012

FFU WAFANYA KWELI “INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL”, TUBINGEN, UJERUMANI.


FFU wa Ngoma Africa Band walipofanya kweli katika maonyesho ya International African Festival, mjini Tubingen,Ujerumani siku ya jumamosi
11.08.2012, Pia maonyesho hayo yaliambatana na sherehe za tuzo la “IDA- International Diaspora Award” mshindi wa Tuzo hiyo ni Ngoma Africa band, ambayo imechaguliwa kuwa ndio bendi bora ya kiafrika iliyofanya kazi nzuri ya kuutangaza mziki wa kiafrika kwa kasi na kujizolea mamilioni ya washabiki katika kila kona duniani. Tuzo hiyo ya “IDA-International Diaspora Award” ambayo imekabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja wa FFU. More info at http://www.ngoma-africa.com/

No comments: