Aug 11, 2012

CHAMA CHA WALIMU KINASEMA HUYU MBUNGE NDIO ANANJAMA ZA KUKISAMBARATISHA


Gratian Mukoba.
Chama cha walimu nchini CWT kimesema kimebaini kuwepo njama za siri za kukisambaratisha ambazo zinaratibiwa na kikundi cha watu ambao hawakuridhishwa na mgomo wa walimu ulioitishwa na chama hicho hivi karibuni huku kikiitaka serikali kuwarudishia madaraka wakuu wote wa shule mbalimbali waliovuliwa nyadhifa zao kutokana na mgomo huo.
Rais wa CWT Gratian Mukoba amemtaja mbunge wa Sumve Richard Ndasa kuwa miongoni mwa watu wanaopanga njama hizo kutokana na madai yake kuwa CWT inabakiza zaidi ya shilingi bilioni 7 makao makuu kwa matumizi yao binafsi madai ambayo hayana ukweli wowote.
Mukoba amesema kutokana na tuhuma zilizotolewa na mbunge huyo, chama kimewasilisha rasmi malalamiko yake kwa spika wa bunge kikimtaka mbunge huyo kuthibitisha hayo madai.
Kwenye line nyingine Mukoba amesema “yani mbunge Richard Ndasa amesimama bungeni na karatasi sijui anaziokota wapi anasema kwamba chama cha walimu kinabakiza bilioni 7 makao makuu akina Mukoba wanagawana, yeye kwanza hajui mapato yetu kwa mwezi ni kiasi gani, hajui hela zetu zinagawanywaje kwenda kwenye wilaya mpaka kwenye shule, hajui vitu ambavyo vinafanywa na hela za chama, anatamka tu tena na karatasi anajifanya anasoma”
Ishu nyingine ambayo Mukoba ameizungumzia ni kuhusu CWT kutoridhishwa na kitendo cha baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya kuwaondoa walimu kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kuanza usiku wa kuamkia augost 26 2012.
Amesema “inaonekana hayo ni maagizo kutoka kwenye ofisi ya waziri mkuu ambapo kabla ya kuwaondoa serikali iliorodhesha majina ya walimu waliogoma na viongozi wa CWT kwa maelekezo yaliyotolewa na Mwalimu Jumanne Sagimi kaimu katibu mkuu Tamisemi, mikoa iliyoathirika sana na zoezi hilo la Sagimi ni Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Iringa n.k ambapo walimu watatu wa shule ya sekondari Mererani waliondolewa kwenye chumba cha mafunzo ya sensa ya watu na makazi kwa maelekezo kuwa walishiriki kwenye mgomo”
Kuhusu hii ishu ya walimu kuondolewa kwenye sensa nakumbuka Waziri mkuu alizungumza bungeni zaidi ya siku tatu zilizopita kwamba, toka mwanzo haikua imepangwa walimu pekee ndio watasimamia zoezi la sensa, sasa hivi kuna vijana waliomaliza elimu ya sekondari na vyuo lakini hawana kazi mtaani.
Unaaweza kumsikiliza Mukoba hapo chini… kwenye sauti ya kwanza anamzungumzia huyu Mbunge na sauti ya pili anazungumzia walimu kupigwa chini kwenye tenda ya kusimamia sensa.

No comments: