Aug 12, 2012

AY HUYOOOOOOOOO............

Ay, Lamyia na Hemdee…. Kama haufahamu, kolabo ya kwanza ambayo haikutoka ya Ay na Sean Kingston ndio ilimfanya Ay kuombwa kolabo na Lil Romeo na Lamyia Good baada ya kuisikia studio huko Marekani.
Naona siku zinahesabika na zimebaki chache kwa ajili ya Ay kuchukua pipa moja kwa moja mpaka Los Angeles Marekani kwa ajili ya kufanya ile project kubwa ambayo kila alieisikia taarifa yake zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekua na hamasa ya kusikia nini kinaendelea.
Mwimbaji Staa Sean Kingston alipokuja bongo mwaka juzi alitangaza kupitia XXL ya CLOUDS FM  kwamba yuko tayari kufanya kolabo na Mtanzania Ay ambapo siku kadhaa mbele, Ay alinisikilizisha wimbo wake aliorekodi Marekani ambayo ndio kolabo na Sean Kingston.
Ulipita muda wa ukimya kidogo baada ya Ay kurekodi audio ya kolabo ya kwanza na Kingston ambayo ndio alinisikilizisha, ukimya ulifata baada ya hapo lakini kumbe Ay alikua anavuta subira na kuongeza uvumilivu kutokana na ratiba nzito ya Kingston ambae alikubali kufanya nae kolabo bure, wakati Jose Chameleone wa Uganda kwenye kolabo aliyoahidiwa na Sean Kingston ameambiwa atailipia USD elfu 30 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kibongo.
Ay amesema “Marekani nakwenda September 2012 kufanya kolabo na Tyga wa Cash Money pamoja na video na Sean Kingston, hizi kazi zinahitaji hela  lazima uwe unajipanga kwelikweli yani ukienda unafanya kazi unamaliza unarudi zako”
Los Angeles.
Millard Ayo alipomuuliza kama amekamilisha kolabo kwa upande wa audio na Sean Kingston, Ay amejibu “unajua mimi na Sean tumerekodi nyimbo mbili, tulirekodi nyimbo ya kwanza ambayo wewe ndio uliisikia nakumbuka baada ya hapo walipoona ‘party zone’ akasema eeehhhhh uko serious eeh? ile ya kwanza tuachane nayo ngoja tufanye kitu kingine kizuri zaidi na kusema kweli ukisikiliza wimbo wa kwanza na wimbo wa pili, wa pili ni mzuri zaidi na ndio ambao tunashoot”
Ambwene amesema kwa sasa hawezi kutaja jina la hiyo new single ya pili lakini video itafanyika Las Angeles, producer ni yule yule alierekodi ‘speak with your body’ na ndio anaefanya kazi za Sean Kingston, za Soulja Boy, ni injinia wa Akon na Lady Gaga pia.
Video ya ‘party zone’ ya Ay iliyomshawishi Sean kubadili maamuzi ilipelekwa kwake june 2012 na meneja wa Ay ambae ni Hemdee mwenye mchanganyiko wa Mganda na Mmarekani ambapo ilimfanya Sean Kingston kurekodi hiyo kolabo ya pili mwishoni mwa mwezi wa sita.
Unaweza kumsikiliza Ay mwenyewe akiongea hapo chini, chini yake pia kuna sauti ya Sean Kingston akimzungumzia Ay.

No comments: