
Wanamuziki wa Pop wa kike wakiongozwa na Taylor Swift, Rihanna na Lady Gaga wametawala orodha mpya ya jarida la Forbes la maceleb wanaolipwa pesa nyingi zaidi wakiwa na umri wa chini ya miaka 30.
Swift, 22, amempiga fimbo Justin Bieber katika nafasi ya kwanza kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 57 kwa mwaka hadi kufikia mwezi May mwaka huu (May 2011 – May 2012).
Mrembo huyo hulipwa dola milioni moja kwa kila concert anayopiga.

Bieber, 18, amekamata nafasi ya pili kwa kuingiza dola milioni 55 alizozipata kwa kuuza nyimbo, concerts na matangazo ya bidhaa kama lotion za Proactiv.

Rihanna, 24, amemzidi mshindi wa kwanza wa mwaka jana Lady Gaga katika nafasi ya tatu kwa kuingiza dola milioni 53.
Mwanamuziki huyo wa Barbados ameingiza hela hizo kutokana na albam yake ya “Talk That Talk”, tour yenye show 85 aliyofanya na matangazo kama ya Vita Coco coconut water na Nivea lotion.

Gaga, 26 amekatama nafasi ya nne kwa kuingiza dola milioni 52 chini sana ya dola milioni 90 alizoingiza kabla ya hapo.

Katy Perry, 27, na Adele, 24, wamekamata nafasi ya tano na sita kwa kuingiza milioni 45 kwa Perry na dola milioni 35 kwa Adele.
![]() |
| Adele |
Muigizaji wa kike Twilight” Kristen Stewart, rapper Lil Wayne na waigizaji wa kiume wa “Twilight” Taylor Lautner na Robert Pattison wamekamilisha list kwa kuingiza kati ya dola milioni 26.5 na milioni 34.5.
![]() |
| Kristen Stewart |
![]() |
| Robert Pattison |
![]() |
| Taylor Lautner |




No comments:
Post a Comment