Feb 24, 2012

Beef jipya kati ya Chris Brown na mwana masubwi CM PUNK


Hii ni baada ya mtu mzima Chris Brown kuachia RMX na Ex Girlfriend Rihanna katika nyimbo ya mwanadada huyo unayoitwa "Birthday Cake" brizzy aliandika katika ukurasa wake wa twitter kua "wote waliomsema vibaya wao sio mungu makosa yanatokea kwakila binadamu" sasa moja kati waliowaigi kumsema vibaya Chris Brown hadharani ni mwana myeleka ambae ni Bigwa wa WWE anaejulikana kama CM PUNK ambapo aliandika pia kwenye twitter kua "Kama kweli Chris Brown anapenda kupiga watu mbona hajampiga mtu anaejua kupigana?...Baadae Chris alijibu kwa kusema kua hamna lolote CM PUNK anataka kupata umaharufu zaidi kwenye twitter kupitia jina lake na kumdharau kwa kusema kama ndo hivyo basi awasiliane na msaidizi wake ili aweze kumpa picha kubwaaaaa kama mshabiki wake namba moja kwenye muziki wake....
Baada ya hapo Mwana masumbwi huyo ali post  video kwenye mitandao ya kijamii.......


Na baada ya Chris Brown kuiangalia video hiyo ambayo alidisiwa kinoma noma aliweza kumjibu CM PUNK kama ifatavyo...
"@cmpunk video ulionitumia ni nzuri inaonesha ni jinsi gani unavyojiamini na ukweli ni kua sikujui kwa hiyo cha kuchekesha ni sitojali hata kidogo ulichokiongea kwasababu sikujui na natumaini kua dakika 15 ulizotumia kuni diss kwenye video hiii zitakua zimeshakupa umaarufu kwasababu muziki unabaki milele na wanamasubwi wanakuja na kuondoka"
hayo ndo maneno ambayo Chris Brown alimalizia......

No comments: